24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

VYUO BORA KWENYE TAALUMA YA UCHUMI DUNIANI

Na FARAJA MASINDE,

KWA nchi kama Tanzania unapotaja vyuo vinavyotoa taaluma ya uchumi basi lazima utakigusa Chuo Kikuu cha Biashara Dar es Salaam (UDBS), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Taasisi ya Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo Kikuu cha Mzumbe na vingine vingi.

Hata hivyo, licha ya kuwapo kwa vyuo hivyo bado haijawa kigezo kwa wanafunzi wa Kitanzania kutovuka mipaka na kwenda kusoma nje ya nchi, kwenye vyuo vikuu vilivyojiimarisha kitaaluma kwa lengo la kujiongezea ujuzi katika taaluma hii ya masuala ya uchumi na fedha kwa ujumla.

Inafahamika kuwa kila nchi duniani ina vyuo vikuu bora kwenye fani mbalimbali, jambo ambalo muda mwingi huchanganya wanafunzi wengi pindi wanapohitaji kwenda kusoma ng’ambo kwa kushindwa kujua kuwa ni nchi gani bora yenye chuo anachostahili.

Kwa sababu ya changamoto hiyo, ndiyo maana kumekuwapo mashirika mbalimbali ambayo yamejikita katika kuhakikisha kuwa yanatoa orodha na takwimu juu ya vyuo unavyoenda kusoma kwa ajili ya fani husika.

Fani kama kilimo, udaktari, ualimu, uchumi, uhandisi ni moja tu ya zile ambazo vyuo vyake vimeorodheshwa tayari ambavyo mwanafunzi anaweza kwenda kuongeza ujuzi wake ili kufika mbali zaidi ikiwamo pia kumsaidia kutambulika kimataifa na hata kupata kazi nje ya nchi jambo ambalo limekuwa ni miongoni mwa malengo ya watu wengi.

Kama hivyo ndivyo, leo tunaangalia vyuo vikuu ambavyo ni  bora kwa ajili ya mwanafunzi  kupata taaluma ya masuala ya uchumi duniani.

Utafiti huu umetolewa na Shirika la utafiti wa vyuo vikuu duniani kwenye upande wa taaluma la QS, ambalo limevitaja vyuo vikuu bora kwenye utoaji wa taaluma katika fani ya uchumi duniani. Orodha ambayo  itakuwa ni msaada mkubwa kwako mwanafunzi unayefikiria kwenda kusomea masuala ya uchumi kuweza kujua uende na mwelekeo upi kwa mwaka huu.

Kama ilivyo ada ya QS, utafiti umekuwa ukitazama nyanja nyingi ikiwamo tafiti pia namna ambavyo wanafunzi wake wamefanikiwa kuajiriwa kirahisi dunani kote, huku eneo jingine likiwa ni lile la utoaji wa taaluma hii ni pamoja na namna ambavyo wahitimu wake hata mara baada ya kuajiriwa utendaji kazi wao umekuwa ni wa kiwango gani.

Kwenye orodha hiyo ambayo kama ilivyo ada Marekani imeendelea kuongoza kwa kuwa na orodha kubwa ya vyuo ikifuatiwa na Uingereza.

Chuo kilichoshika nafasi ya kwanza ni Massachusetts Institute of Technology (MIT), nafasi ya pili ni Harvard, nafasi ya tatu ni Stanford huku nafasi ya nne ikichukuliwa na Chuo kikuu cha Princeton vyote kutoka nchini Marekani.

Kwenye nafasi ya tano kuna Chuo Kikuu cha California, Berkeley (UCB) huku namba sita ikichukuliwa na Chuo Kikuu cha Chicago vyote kutoka nchini Marekani.

Vyuo vikuu vingine kwenye nafasi ya saba ni London School of Economics and Political Science (LSE) nafasi ya nane ni Chuo Kikuu cha Oxford vyote hivi ikiwa ni kutoka nchini Uingereza. Vyuo bora vya uchumi katika nafasi ya tisa ni Chuo Kikuu cha Yale nchini Marekani na katika nafasi ya kumi ni Chuo Kikuu cha Cambridge nchini Uingereza.

Hii inaonyesha wazi kuwa katika utafiti huo vyuo vikuu vilivyong’ara ni kutoka nchini Marekani ikifuatiwa na Uingereza, nchi ambazo zimeweza kuwa na vyuo vikuu vingi kwenye orodha hiyo inayohusu masuala ya uchumi.

Hata hivyo, kwenye nafasi ya kwanza na ile ya pili kumekuwa na mvutano baina ya vyuo hivi viwili ambapo hata hivyo ubora wa kila kimoja hadi kushika nafasi ya kwanza imekuwa ikitegemeana na shirika la utafiti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles