25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

‘Vyombo vya majini visivyogaguliwa marufuku kufanya kazi’

NA OSCAR ASSENGA, TANGA

SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania mkoani, limesema vyombo vya majini ambavyo havijakaguliwa na kupata cheti cha ubora haviruhusiwi kwenda majini kufanya shughuli zake. 

Agizo hilo lilitolewa jana na Ofisa Mfawidhi wa Shirika la Uwakala wa Meli Mkoani Tanga (Tasac) Christopher Shalua wakati akizungumza na gazeti la MTANZANIA ofisini kwake.

Alisema wao wanatoa wito kwa vyombo vya majini kwa kipindi hiki cha masika vyombo ambavyo havijakaguliwa na kupata cheti cha ubora haviruhisiwi kwenda majini.

 Alisema kwa kipindi hicho vyombo vyote vilivyopata vyeti vya ubora ni vizuri kuchukua tahadhari kuhakikisha vifaa vyote vya umuhimu ikiwemo pampu za kutolea maji yaliyoingia kwenye chombo zinafanya kazi na zipo.

Aidha alisema kwa vyombo ambavyo na vyombo havitakuwa na vifaa vitakavyostahili kuruhusu kwenda majini wanavitaka visienda kufanya shughuli zozote majini kwa kuchukua tahadhari.

“Tunatoa rai kwa vyombo vizingatia maelelezo hayo kwa sababu kipindi cha masika kinaambatana na hali mbaya ya hewa mawimbi makubwa pamoja na mvua ambazo zinasababisha maji kuingia kwenye chombo na kusababisha uzito,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles