25.2 C
Dar es Salaam
Saturday, January 29, 2022

VYETI FEKI VYATIKISA SEKTA YA AFYA

*Sumaye avunja ukimya kwa viongozi


Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM

SEKESEKE la orodha ya watumishi walioghushi vyeti limepamba moto huku sekta ya ya afya ikitikiswa zaidi.

Huku hali ikiwa hivyo,  Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, ameweka wazi suala zima wa uhakiki wa vyeti na akitaja sifa ya kiwango cha elimu inayotakiwa kwa wakuu wa mikoa na wilaya.

Sumaye alisema  mabadiliko hayo yalifanywa na Serikali ya Awamu ya Tatu wakati yeye akiwa  waziri mkuu na msimamizi mkuu wa shughuli za Serikali.

Orodha iliyochapishwa kwenye baadhi ya magazeti jana ilionyesha watumishi wa kada mbalimbali ambao wanadaiwa wamekuwa wakitumia vyeti vya kughushi kinyume cha sheria.

Wakati hayo yakiendelea, Zahanati ya Kibada katika  Manispaa ya Kigamboni, Mkoa wa Dar es Salaam ilitajwa kuwa  watumishi wake wamekumbwa na tatizo hilo, hali iliyochangia huduma kuzorota kwa wagonjwa.

MTANZANIA ilifika   katika zahanati hiyo  jana na kumkuta muuguzi  mmoja tu ambaye alisema  zahanati hiyo haijafungwa.

Hata hivyo alisema  uhakiki huo umewakumba wenzake  watatu ingawa idadi kubwa bado walikuwa wakiendelea na kazi kwa mujibu wa utaratibu.

“Si kweli, hatujafunga zahanati, huduma inaendelea kutolewa kama kawaida.

“Kwa kuwa   hiki ni kituo kidogo cha afya siku za mwishoni mwa wiki (Jumamosi na Jumapili) baadhi ya idara huwa zinafungwa mapema.

“Pengine wakadhani ni kwa sababu ya vyeti feki, si kweli ni hali ya kawaida,  ingawa  idara hizo zinawahi kufungwa haimaanishi mgonjwa akija ahudumiwi, anahudumiwa kama kawaida maana kuna huduma za dharura,” alisema.

Alisema katika kituo hicho wapo wataalamu zaidi ya 10 na   katika orodha   iliyotolewa na serikali ya wenye vyeti vya kughushi, yamo majina matatu ya wenzao.

“Tumeona majina ya wenzetu watatu  kwa kweli hata sisi tumeshangaa, bado hatuamini kama ni wao, tunaona pengine kuna  ‘typing error’ (makosa ya uchapaji)…  huwezi jua naamini serikali ipo makini katika utendaji wake,” alisema muuguzi huyo.

MTANZANIA lilihitaji kuonana na Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo kupata ukweli zaidi lakini hakuwapo ofisini kwa muda huo. 

Sumaye

Wakati huohuo, Waziri Mkuu mstaafu wa Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye, ameweka wazi suala la uhakiki wav yeti feki, alipohojiwa katika  kipindi cha  Uchumia,  Siasa na Utamaduni cha redio moja ya   Dar es Salaam.

  Alisema akiwa bado Serikalini katika awamu ya tatu yalifanyika  mabadiliko  kuhusiana na taratibu za utumishi wa umma kwamba kwa wakuu wa mikoa na wa wilaya,   lazima  viwango vyao vya elimu vianzie  Shahada ya Kwanza.

“Nakumbuka katika nafasi ya kuwakilisha watu kama vile wabunge na madiwani ndiyo  wanaosema hivyo, kwamba mtu awe anajua kusoma na kuandika, kama wananchi wanawaona wanaweza kutafsiri  vizuri na kuwaletea kile walichowatuma  kutoka bungeni au kwenye halmashauri.

“Lakini nakumbuka katika taratibu za utumishi siyo hivyo, hayo mabadiliko yalifanyika katika awamu ya tatu…najua katika taratibu za utumishi tulikubaliana  kuwa mkuu wa wilaya lazima awe na digrii na ni mahitaji la nafasi hiyo kwa sababu  pamoja na kuwa ni  shughuli za  siasa pia anasimamia shughuli za utendeji ambazo nyingi ni shughuli utaalamu za Serikali.

“Hivyo hauwezi kusema DC na RC awe anajua kusoma na kuandika…kusema awe anajua kusoma na kuandika tu,” alisema

Alisema pengine walifanya hivyo wakati wa uhuru, lakini anachojua walifanya mabadiliko.

Sumaye alisema  kwenye nafasi za utendaji kama mkuu wa wilaya na RC hauwezi kubadilisha,   hivi sasa hata makatibu tarafa wengi ni wale waliomaliza chuo kikuu.

Alisema akiwa serikalini kama Waziri Mkuu ulipitishwa utaratibu ambao  mkuu wa wilaya lazima awe na shahada ya kwanza.

“Haiwezekani leo katika umri huu tuseme mkuu wa mkoa awe anajua kusoma na kuandika. Hivi kweli inaingia hata akilini?

“Hapa ni kwamba kilichofanywa ni kumlinda mtu fulani.

“Hatuwezi kuwa na utaratibu kwamba mradi mtu akiwa anajua kusoma na kuandika anaweza kuwa mkuu wilaya na mkoa… hata kuwa katibu tarafa hatufai,” alisisitiza  Sumaye.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
177,207FollowersFollow
532,000SubscribersSubscribe

Latest Articles