23.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

VYAKULA VINAVYOHATARISHA NGUVU ZA KIUME

soda
Soda

 

Na MWANDISHI WETU,


TATIZO la nguvu za kiume linazidi kuwasumbua wanaume wengi hapa nchini. Wengi wamekuwa wakilalamikia tatizo hilo na kutafuta njia mbalimbali za kukabiliana nalo.

Madaktari wamekuwa wakitoa ushauri wa aina mbalimbali kuhakikisha kuwa vijana wanaondokana na hali hiyo, lakini wanagonga mwamba. Hii ni kutokana na mfumo wa maisha walionao vijana wengi hasa katika masuala ya vyakula na kuendekeza ulevi.

Leo MTANZANIA imeona ni vema ikaandika makala hii inayohusu vyakula ambavyo kwa kiasi kikubwa vinachangia upungufu wa nguvu za kiume… ili iwapo itawezekana watu waviepuke. Baadhi ya vyakula hivyo ni vile vyenye asili ya homoni ya kike iitwayo estrogen.

Mbegu za kitani (Flax seeds)  

Ni muhimu mno kufahamu aina ya vyakula ambavyo si rafiki kwa wanaume katika kuongeza kiwango cha homoni ya kiume iitwayo testosterone. Homoni hii huchochea sifa ya mwanamume yaani kuwa na nguvu za kiume.

Vyakula vinavyotengenezwa na unga wa mbegu za kitani (flax seeds) vimekuwa vikisifiwa kwa kuwa Omega-3 fats ambayo ni muhimu mwilini. Mbegu hizi zinasifika kwa kuwa na estrogen ambayo ni sawa kabisa na homoni ya estrogen iliyoko katika mwili wa mwanamke.
Mbegu hizi zina kiwango cha phytoestrogens mara tatu zaidi ya soya.

Licorice (susu)

Huu ni mzizi ambao hutumika hasa kuondoa tatizo la msongo (stress) kwa watu wanaokumbwa na tatizo hilo. Pia hutumika kama sukari kwenye chai au kahawa badala ya kutumia sukari ya kawaida.
Mzizi huu una estrogen ambayo hushusha kiwango cha homoni ya kiume ya testosterone kwa wanaume.

Utafiti ulifanywa na jopo la wataalamu wa masuala ya afya ambapo wanaume saba wenye afya walipewa gramu saba za vidonge vya licorice kila mmoja kila siku.
Vidonge hivyo vilikuwa na kiasi cha gramu 0.5 za glycyrrhizic (kiambata kilichomo ndani ya licorice kinachopunguza testosterone kwa mwanamume). Baada ya siku nne tu kiasi cha homoni ya testosterone kwa kila mwanamume aliyefanyiwa utafiti huo kilipungua kwa kiwango cha nusu ya kiasi cha homoni kwa kila mwanamume tofauti na kilivyokuwa wakati wa kuanza utafiti.

Bia

Kinywaji hiki kimetengenezwa kwa humle (hops) ambayo kwa kiwango kikubwa inaleta hali ya homoni za kike kwa wanaume (highly estrogenic). Humle  ina kiasi cha 300,000 IU cha estrogen kwa kila gramu 100. Kabla ya mwaka 1487 bia ilikuwa ikitengenezwa kwa viambata (ingredients) ambavyo vililenga kumfanya mwanamume anapoinywa awe na hali ya uanaume kweli kweli (more aggressive, horny and socially dominant).
Baadaye kanisa liliingilia kati uzalishaji wa bia na kutaka itengenezwe kwa viambata ambavyo vitamfanya mwanamume awe mpole au mtaratibu na si mtu wa maguvu na ubabe. Hapo ndipo likazaliwa wazo la kutengeneza bia kwa kutumia humle. Siku hizi bia hutengenezwa kwa viambata vitatu, humle, maji na malt.

Soya 
Hii ina kiwango kikubwa cha ‘Isoflavones’ ambayo kiuhalisia ni estrogen. Ulaji wa soya ni sawa na kula kidonge kimoja cha uzazi wa mpango.

Spearmint

Hutumiwa zaidi kama kiambata kwenye bazooka, dawa ya meno na hata majani ya chai (herbal tea). Pia ina kiwango kikubwa cha estrogen.

 Lima beans (Fiwi) 

Yana homoni za kike (estrogen) iitwayo ‘inositol’ ambayo hupunguza kiwango cha homoni ya kiume.

Soda 

Chupa za plastiki ambazo hutumiwa na kampuni zinazotengeneza soda zimetengenezwa kwa ‘phthalates’ ambayo hufanya plastiki ziweze kukunjwa katika umbo lolote (flexibility).

Phthalates ni estrogen! Kawaida ili kuondoa phthalates kwenye chupa za plastiki kampuni zinapaswa kuziacha chupa hizo zikae kwa mwaka mmoja bila kuweka soda ndani yake. Lakini wao wanachokifanya ni kwamba mara tu baada ya kutengeneza chupa hizo huweka soda ndani yake na kuzipeleka sokoni kwa walaji.
Matokeo yake phthalates huingia kwenye soda hivyo pindi mwanamume anapoinywa unaingiza homoni za kike mwilini mwake ambapo matokeo yake ni kupunguza homoni za kiume.

Fast food

Vyakula vinavyotengenezwa kwenye migahawa ya aina hii hasa vile vya nyama vimetokana na wanyama waliofugwa na kupewa dawa za antibiotics na homoni za kukuzia wanyama ambavyo vyote hivyo vina asili ya homoni za kike. Nyama hizo zinakaangwa au kupikwa kwa mafuta ya mimea ambayo yana estrogen. Hivyo mwanamume anapokula ni rahisi kuwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Makala hii imeandaliwa kwa msaada wa blogu ya Asili yako.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles