23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Vyakula kuongeza nguvu za kiume, sababu ya kushiriki ngono

MWANDISHI WETU

SIKU hizi vijana wengi wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la nguvu za kiume. Sababu zinazotajwa ni nyingi, lakini kubwa zaidi ni mtindo wa maisha unaojumuisha vyakula, ambavyo vimekuwa chanzo kikuu cha maradhi yanayoua nguvu za kiume. Hata hivyo, wataalamu wa masuala ya afya wanasema kuwa vipo vyakula ambavyo husaidia kuimarisha tendo la ndoa na kuzidisha hamu ya tendo.

Wanasema lishe bora, kufanya mazoezi na afya nzuri ya akili vyote kwa pamoja vinaweza kuimarisha tendo la ndoa.

Viungo vinavyoweza kuchochea hisia ya furaha – kutokana na homoni ya endorphins, vina virutubisho vinavyohusishwa na kuimarika kwa tendo la ndoa, au kwa jumla vinahusishwa na ufanisi wakati wa kushiriki tendo hilo.

Vyakula vinavyotajwa kuimarisha tendo la ndoa

Wapo baadhi ya watu wanaodai kwamba ulaji wa chaza husaidia kuimarisha tendo la ndoa hata hivyo, hakuna aliyethibitisha kwamba ulaji wa chaza una uhusiano na kuongezeka kwa tendo la ndoa.

Simulizi au ngano za kale zinaeleza kwamba wakati Aphrodite – Mungu wa tendo la mapenzi – alipozaliwa kutoka povu jeupe na kufufuka kutoka baharini, ndipo chakula cha baharini kilipoonekana kuwa ni kichocheo cha kuimarisha tendo la ndoa.

Lakini, habari nzuri kwa wanaopenda kula chaza ni kwamba wana madini ya zinc ambayo ni kirutubisho muhimu kinachotumika kuunda homoni ya testosterone.

Utafiti umebaini kwamba zinc inaweza kusaidia kutibu matatizo ya wanaume wasioweza kuzalisha, pia husaidia kuboresha manii.

Vyanzo vingine vizuri vya zinc hupatikana katika nyama nyekundu, mbegu za tango, korosho na lozi, lakini pia kwenye maziwa na hata jibini.

Chokoleti

Utafiti unabainisha kuwa ulaji wa chokoleti nyeusi unaweza kumpa mtu hisia ya awali pindi anapompenda mtu, hii ni kwa sababu ina ‘kemikali ya mapenzi’ phenylethylamine (PEA).

PEA – ambayo huwapo katika miezi ya kwanza ya uhusiano, huchangia kuwapo kwa homoni inayomfanya mtu kujihisi vizuri na kuchochea raha katikati ya ubongo wake.

Chokoleti

Ni kiwango kidogo tu cha PEA kilichopo katika chokoleti, lakini kuna shaka iwapo kiwango hicho kinaendelea kuwapo wakati wa kuliwa.

Cocoa pia ina amino acid tryptophan, ambayo inasemekana huongeza msukumo wa damu na viwango vya serotonin (homoni nyingine ya furaha).

Hivyo basi, uhusiano baina chokoleti na tendo la ndoa huenda ulianza katika karne ya 16.

Hernán Cortés, ambaye alikuwa mtawala wa Kihispania katika karne hiyo, aliyeidhibiti Mexico wakati huo, chini ya ufalme wa Castile, inadhaniwa ndio raia wa kwanza barani Ulaya kugundua chokoleti.

Cortés alimuandikia barua mfalme akimweleza kwamba amegundua kinywaji cha cocoa kinachosaidia ‘kuimarisha kinga na kukabiliana na uchovu.’

Lakini raia wa zamani wa Castile, huenda walihusisha nguvu hizo na chokoleti na hakuna ushahidi kwamba kweli huimarisha tendo la ndoa.

Pilipili nayo yatajwa

Vijana wengi wa sasa, wake kwa wa waume wameaminishwa kwamba pilipili ni kichocheo kizuri cha tendo la ndoa.

Pilipili ambazo zinatajwa kuwa na kichocheo kinachojulikana kwa jina la kitaalamu Capsaicin, ambayo utafati umebaini kuwa inaweza kuchochea homoni ya endorphins (ya kujihisi furaha), imekuwa ikipendwa na watu wengi wanaotamani kufurahia ngono.

Pilipili

Pilipili pia inatajwa kusaidia kuharakisha ufanyaji kazi wa mfumo wa kusaga chakula tumboni, kuongeza joto mwilini na kasi ya mapigo ya moyo, mambo ambayo huhisiwa wakati wa tendo la ndoa.

Vijana wengi wanaokula pilipili kwa wingi, husema kuwa miili yao huwa na joto zuri hivyo hata wanaposhiriki ngono huwafurahisha wapenzi wao.

Pia huwaongezea hamu ya tendon a hivyo kujikuta wakitamani kuwa na wenza wao mara kwa mara.

Pombe husaidia au hutatiza?

Watu wengi wanaokunywa pombe hutamani kushiriki tendo la ndoa wakati mwingine hata na mtu yeyote aliye karibu yake.

Pombe inatajwa kuongeza hamu na kumfanya mnywaji ashindwe kujizuia. Hata hivyo, asilimia kubwa ya watu wanaokunywa pombe kupita kiasi, hupata hamu ya tendo lakini hushindwa kutekeleza kwa ufasaha, tofauti na wale wanaokunywa kiasi bila kulewa.

Mara nyingi hisia hupungua kwa wanaume na wanawake wanaokunywa pombe nyingi, na katika kipindi cha muda mrefu inaweza kupunguza uwezo wa kushiriki tendo la ndoa na hata wakati mwingine kushindwa kabisa kushiriki tendo hilo.

Ubaya unakuja zaidi pale ambapo mmoja kati ya wenza hao hanywi pombe kabisa, kwani harufu huwa haimvutii na hivyo kushindwa kutoa ushirikiano wakati wa tendo.

Vichochezi vya kuongeza hamu

Vichochezi vinaweza kugawanywa katika makundi matatu: Vinavyoshughulikia hamu, uwezo wa kushiriki tendo na raha inayotokana na tendo lenyewe.

Hakuna vilivyothibitishwa kisayansi kuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa binadamu kutokana na ugumu wa kupima ufanisi wake.

Ni harufu ya kuiva na kuoza kwa tunda pekee ndiyo iliyoweza kuthibitishwa, na hufanya kazi kwa wadudu wa matunda wanaoruka.

Dk. Krychman, Mtaalamu wa afya ya ngono, anasema anadhani watu hula vichochezi hivyo kwa sababu ya imani kwamba vitafanya kazi, lakini hawajiulizi vinasaidiaje na kwanini vinafanya kazi.

Vichochezi vingi huwa ni vinywaji, lakini wataalamu wanashauri kuepuka kunywa dawa zinazotokana na mimea ambazo hazijathibitishwa kitaalamu kwamba hazina madhara kiafya.

Matatizo kiafya

Asilimia kubwa ya vijana wenye matatizo ya kukosa hamu ya tendo la ndoa, mara nyingi hukabiliwa na maradhi ya hapa na pale au msongo wa mawazo.

Hivyo, madaktari wanashauri iwapo mtu amekosa hamu ya tendo la ndoa kwa muda mrefu au ana upungufu wa nguvu za kiume ni vema akaonana na wataalamu waweze kumpatia ushauri nasaha au tiba iwapo afya yake haiko sawa.

Kwanini watu wanashiriki tendo la ndoa?

Watu wengi leo hii ukiwauliza kwanini wanashiriki tendo la ndoa, sababu watakayokupa ni kutafuta watoto.

Majibu haya yanatokana kwamba tendo hili linahusisha zaidi kutafuta watoto, pia ni kwa sababu watoto hupatikana kwa njia hii.

Lakini je, wangefikiria nini kuhusu tendo la ngono iwapo suala la kupata watoto lisingekuwapo?

Tangu kuzaliwa kwa mtoto wa kwanza wa maabara mwaka 1978, takriban watoto milioni nane wamezaliwa kupitia mfumo wa kiteknolojia wa IVF, ambapo yai la mama na mbegu za kiume huchanganywa nje ya kizazi cha mama anayebeba mimba kabla ya kutungwa katika kizazi chake.

Na idadi hiyo huenda ikaongezeka katika siku zijazo, huku vifaa vya kubaini hatari ya magonjwa ya jeni katika viini tete ikiwa kitendawili.

Ukweli ni kwamba, hata katika siku za usoni ambapo watoto wengi zaidi wanaweza kuzaliwa bila wazazi wao kushiriki tendo la ndoa, bado wanandoa watafanya ngono hata kama lengo lao si kutengeza watoto.

Henry T Greely, aliyetunga kitabu cha The End of Sex And The Future of Human Reproduction, anasema katika kipindi cha kati ya miaka 20 na 40, watu wengi duniani walio na afya njema watachagua kupata ujauzito katika maabara.

Kitabu cha Greely kwa sasa kinatathmini baadhi ya changamoto zinazokabili mpango huo wa kimaabara.

Kwa sasa, kutakuwa na ukosoaji wa hali ya juu lakini kadiri siku zinavyosonga mbele huku watoto wanaokuzwa katika maabara wakionekana kuzaliwa bila kukabiliwa na tatizo lolote hasa la kuwa na vichwa viwili au mkia, umma utapendelea kupata watoto kupitia njia zisizoshirikisha tendo la ngono.

Katika ulimwengu huo, ambapo watoto huzaliwa katika maabara, ujauzito kupitia tendo la ngono utakuwa ni chaguo la mtu, ambapo maadili ya ngono hayahusiani na kutafuta watoto.

 

Lengo la kushiriki ngono

Kibailojia, kuna sababu moja iliyo wazi kuhusu binadamu kushiriki ngono.

Sababu mbili muhimu za watu kushiriki ngono ni kutimiza malengo ya kibaiolojia ikiwamo kutafuta watoto na upendo.

Hivyo basi, watu hushiriki teto hilo kutokana na mapenzi na hisia walizonazo wawili wapendanao.

Aristotle anasema watu hushiriki ngono si kwa sababu wanataka, bali ni kwa sababu wanataka kupenda na kupendwa.

Anasema ngono si kitu bali kitu chengine, kitu kilichopo juu, kitu kizuri.

Kama ilivyo kwa watu wengine, Aristotle anachukulia tendo la ngono kwamba huenda sambamba na mapenzi.

Tofauti iliyopo kati ya binadamu na wanyama ni kwamba binadamu hufurahia zaidi kufanya vitu vibaya, tea wanavifanya huku wakiwa na furaha. Hivyo, ngono hufanywa kwa lengo la kujiridhisha ama kujifurahisha. Ndio maana watu wanapokosa hamu au uwezo huo hukimbilia kutafuta tiba ama vyakula vya kuwafanya kuwa imara.

Utafiti uliofanywa mwaka 2015 na Profesa wa Saikolojia katika Chuo Kikuu cha San Diego, Jean M Twenge, akichunguza tabia za raia wa Marekani kuhusu tendo la ndoa kati ya 1970 hadi 2010.

Aligundua kwamba kati ya mwaka 1970 na 2010, raia wa Marekani walianza kukubali kushiriki ngono nje ya ndoa.

IMAGES

Sambamba na tafiti zilizopita, kupungua kwa imani za kidini na ongezeko la sifa za kibinafsi, Wamarekani wengi wanaaamini kwamba ngono haipaswi kuzuiwa na mikusanyiko ya kijamii.

Vizazi vya hivi karibuni pia vimeanza kuwa na imani kama hiyo, vikiripoti kiwango cha juu cha washirika wa tendo la ngono nje ya ndoa kama vile watu wazima, na wengi wanazidi kushiriki ngono nje ya ndoa zaidi ya wale waliozaliwa mapema karne ya 20.

Twenge anasema kwamba katika idadi ya watu, tabia hutofautiana kwa sababu ya miaka, jinsia, dini na imani, lakini utafiti unaonyesha kwamba mabadiliko makubwa kuhusu tendo la ngono kati ya vizazi yamefanyika kwa muda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles