23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Vodacom Foundation yazindua tovuti ya e-fahamu kuwasaidia wanafunzi

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

Kampuni ya Vodacom Tanzania Foundation imezindua tovuti  ya maswala ya elimu  ya e- fahamu kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ambayo inajumuisha masomo ya Hisabati, Sayansi, Sanaa na Sayansi ya Jamii ambayo itawasaidia wanafunzi kupata vitabu vinavyofuata mitaala kutoka Maktaba ya Taasisi ya elimu na masomo ya kimataifa bure kwa njia ya mtandao.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako.

Akizungumza leo Mei 7, 2021 jijini hapa wakati wa uzinduzi huo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Joyce Ndalichako amesema kupitia e- fahamu wanafunzi wataweza kuongeza ujuzi na maarifa zaidi huku akifurahishwa na jinsi Kampuni ya Vodacom Foundation ilivyoshirikiana na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote kutoa Komyuta na Routers.

Waziri Ndalichako ameiomba kampuni hiyo kuzidi kuongeza vitabu katika tovuti hiyo ili kuweza kuwasaidia wanafunzi kuzidi kujifunza huku akitoa rai kwa kampuni zingine kuiga mfano wa Vodacom Tanzania Foundation  kutumia teknolojia kusaidia jamii.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Vodacom Foundation, Rosalynn Mworia amesema e- fahamu ni tovuti ya maswala ya kielimu inayopatikana mtandaoni bure kwa ajili ya wateja wa Vodacom ambapo amedai ina nyenzo na taarifa muhimu  za kielimu kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ikijumuisha masomo ya Hisabati,Sayansi,Sanaa na Sayansi ya Jamii.

Amesema ili kupata e- fahamu kwenye simu ama Kopyuta  utahitaji kuunganishwa na huduma ya mtandao wa internet ya Vodacom au kutumia WiFI ambapo baada ya hapo mhusika ataweza kuangalia video  za mafunzo ambapo amedai maudhui yanapatikana katika lugha za Kiswahili na Kiingereza ambapo yapo katika muundo wa sauti,video,machapisho ya PDF na mazoezi shirikishi.

Mkurugenzi huyo wa Vodacom Tanzania Foundation,amesema lengo la kutumia e- fahamu ni kuboresha sekta ya elimu ambapo amedai walianza mwaka 2017 na wamewafikia jumla ya wanafunzi 150,000.

Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga,Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Dk. Leonard Akwilapo wanafunzi na wadau wa elimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles