31.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

VODACOM YATANGAZA KUPATA FAIDA

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania, imetangaza ongezeko la faida ya Sh bilioni 170.24 kwa mwaka wa fedha wa 2017/18 kutoka Sh bilioni 47.554, mwaka 2016/17.

Akitangaza hatua hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom, Ian Ferrao amesema faida hiyo imetokana na faida ya uendeshaji wa M-Pesa na data.

Amesema mapato ya M-Pesa yameongezeka kwa asilimia 16.7, hadi kufikia Sh bilioni 291.193 kutoka Sh bilioni 246 mwaka jana ambapo jumla ya Dola za Marekani milioni 17.5 (Zaidi ya shilingi trilioni 39.5) zililipwa kupitia M-Pesa.

“Manunuzi ya data, yameongezeka kwa asilimia 34.7 ya Sh bilioni 141.61 kutoka bilioni 105.118 kwa mwaka uliotangulia, wateja wakiongezeka kutoka 882,000 hadi kufikia milioni 7.3, hii ikichagizwa na uwekezaji wa Sh bilioni 159. 7 ambao Vodacom imeufanya kwa ajili ya kutanua utoaji huduma wa Mtandao wa ‘4G’ kwa wateja wake katika mikoa mitano,” amesema.

Ferrao amesema mapato kutoka M-Pesa, Data na ujumbe mfupi pamoja na mapato ya uuzaji wa minara ya Vodacom kwa kampuni ya Helios Towers, yalitosha kuziba pengo lililotokana na kupungua kwa upigaji simu kutoka kwa wateja wa kampuni hiyo.

“Tunapoendelea mbele, tunaamini kwamba wateja wetu wa M-Pesa watazidi kuongezeka haswa kwa sababu tunazidi kutanua wigo wetu wa M-Pesa kwa kuongeza huduma ya Lipa kwa M-Pesa, hususani kwa kushirikiana na mabenki,” amesema Ferrao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles