25.9 C
Dar es Salaam
Thursday, December 8, 2022

Contact us: [email protected]

VODACOM kuwajaza mamilioni wateja wake kupitia AMSHA NDOTO

*Sh milioni 10 kushindaniwa kila wiki, milioni 5 kila siku

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kampuni ya Mawasiliano ya Simu za mkononi ya Vodacom Tanzania plc imezindua promosheni ya miezi miwili kuelekea msimu wa sikukuu inayofahamika kama “Amsha Ndoto, Amsha Shangwe”.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Philip Besimire (katikati), akionyesha zawadi wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya ‘Amsha Ndoto Amsha Shangwe’ inayowezesha wateja wa Vodacom kujishindia zawadi mbalimbali  kwa kununua vifurushi ikiwa ni kuelekea Msimu wa Sikukuu Dar es Salaam lNovemba 18, 2022. Kulia ni Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni

Kwa mujibu wa Vodacom promosheni hiyo itawapa wateja wa mtandao huo fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo, mshindi mmoja wa Sh 10, 000,000 kila wiki na Sh 1,000,000 kila siku kwa washindi watano.

Vilevile wateja watakuwa na nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo simu janja, TV janja, mifumo ya 5G, bima ya VODA BIMA na usafiri wa bure kupitia Paisha.

Pia wateja wa Vodacom wanaweza kushiriki kwenye promosheni hiyo na kupata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali kwa kufanya manunuzi na miamala kupita M-Pesa kwa kipindi hichi cha promosheni, pamoja na kutumia huduma za usafiri wa Paisha.

Miamala yote itakayofanyika kupitia M-Pesa kwa kipindi hichi cha promosheni itaingia kwenye droo na kumpa mteja nafasi ya kushinda.

Akizunguma kwenye uzinduzi huo Novemba 18, mwaka huu jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania plc, Philip Besiimire amesema Vodacom imekuwa na utamaduni wa kuwatunuku wateja msimu wa siku kuu kuainisha jinsi Vodacom inathamini mchango wao 

Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam Novemba 18, baada ya kuzindua Kampeni ya ‘Amsha Ndoto Amsha Shangwe’ inayowezesha wateja wa Vodacom kujishindia zawadi mbalimbali  kwa kununua vifurushi ikiwa ni kuelekea Msimu wa Sikukuu.

“Msimu wa siku kuu ni muhimu na unahamasa kwetu sote. Tunapata fursa ya kupumzika na kuwa na wapendwa wetu vile vile kutafakari mafanikio yetu ya mwaka wakati tunaweka malengo yam waka ujao. Kipindi hiki kawaida tuna utaratibu wa kutembelea familia zetu na kuwanunulia zawadi, na sisi kama Vodacom familia yetu ni wateja wetu na ndio sababu ndani ya miaka michache iliyopita tulianzisha utaratibu wa kuwapa zawadi wateja wetu ili kufanya msimu huu wa siku kuu uwe wa furaha zaidi kwao,” amesema Bisiimire.

Amesema Vodacom inamatumaini ya kusaidia kufanikisha ndoto za wateja wake hasa kipindi hichi cha msimu wa siku kuu, ametoa wito kwa wateja wa Vodacom kutumia M-Pesa kufanya miamala na kujiongeea nafasi za kushinda zawadi kubwa.

“Inawezekana ulitaka kumiliki gari, kuanzisha biashara, kulipa ada ya shule, kumalizia ujenzi wa nyumba au kwenda kupumzika, sisi Vodacom tungependa kukusaidia kufanikisha ndoto yako . Tunaamini zawadi tutayokupa utasambaa furaha kwa wateja wetu. Masta Shangwe wetu atatembelea nnchi nzima kusambaa upendo na furaha, hivyo tunatoa wito kwa wateja wetu kufikiria mbele zaidi na kuamini kuwa wakiwa na Vodacom,” amesema Bisiimire.

Wasanii wa kitoa burudani ya wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya ‘Amsha Ndoto Amsha Shangwe’ inayowezesha wateja wa Vodacom kujishindia zawadi mbalimbali  kwa kununua vifurushi ikiwa ni kuelekea Msimu wa Sikukuu, Dar es Salaam.

Promosheni hiyo inapatikana kwa wateja wote wa Vodacom ambapo mteja atasema kitu anachotaka kushinda kupitia M-Pesa App au USSD kwa kupiga *150*00# na kuwa kwenye nafasi ya kujishindia mamilioni na zawadi nyingine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,710FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles