28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

VIWAVI JESHI WATISHIA MAZAO NKASI

Na IBRAHIM YASSIN-NKASI


MATUMAINI ya kupata mavuno mengi ya mahindi katika Wilaya ya Nkasi, mkoani Rukwa, yameanza kupotea baada ya wadudu waharibifu wa mazao aina ya viwavi jeshi kuvamia mashamba ya wakulima na kuyaharibu vibaya.

Wadudu hao wamekuwa wakiharibu zaidi mazao ya mahindi kwa kula majani, kitoto cha mahindi na mbelewele kiasi cha mahindi hayo kushindwa kuzaa.

Akizungumza jana na waandishi wa habari, Kaimu Ofisa Kilimo Umwagiliaji na Ushirika wa Wilaya, Permin Matumizi, alisema wadudu hao wameingia wilayani Nkasi bila wakulima kugundua, wakifikiri kuwa ni wadudu aina ya zongoli na walishitushwa baada ya kuona wadudu hao hawafi kwa dawa za kawaida walizozoea kuwaulia wadudu hao.

Alisema baada ya kupata taarifa hizo kwa wakulima, wataalamu walibaini kuwa, wadudu hao ni viwavi jeshi ambao umbo lao ni kama la zongoli na kwa kitaalamu wanaitwa ‘maize stalkborer-heliothisspp’ na kuwa eneo lililoathirika zaidi ni katika vijiji vya Itekesya na Ntemba, vilivyoko katika Kata ya Kate.

Alifafanua kuwa, wadudu hao ni hatari sana na zinahitajika juhudi za makusudi za kuhakikisha wanadhibitiwa mapema ili kuweza kuyanusuru mazao katika msimu huu wa kilimo wa 2017-18, ili baa la njaa lisije kutokea wilayani humo.

Alisema mpaka sasa jitihada za Serikali zimefanyika kuhakikisha dawa za kuulia wadudu hao zinapatikana kwa wingi katika maduka yote ya pembejeo za kilimo na dawa sambamba na wakulima kushauriwa kuwatumia wataalamu wa kilimo katika kukabiliana na wadudu hao.

Matumizi amewataka wakulima kushirikiana na wataalamu wa kilimo kufanya ukaguzi wa kina wa mashamba yote ili kuweza kubaini uwepo wa wadudu hao ili waweze kushirikiana katika kumaliza tatizo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles