23 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Viwanja 421 kupigwa mnada kwa kutolipiwa kodi

Na Sheila Katikula, Mwanza

Serikali  imekusanya zaidi ya Sh million 900 kutokana na madeni ya kodi ya ardhi kwa  wadaiwa sugu huku viwanja 421 vikitarajiwa kuuzwa baada ya wamiliki wake kushindwa kutekeleza wajibu na kukaidi matakwa ya kisheria ya kulipia kodi viwanja hivyo.

Hayo yameelezwa na Kamishina wa ardhi Msaidizi Mkoa wa Mwanza, Elia Kamihanda wakati akizungumza na  waandishi  wa habari  katika mwendelezo wa kukusanya fedha hizo za kodi kutoka kwa wadaiwa  hao mkoani hapa.
Alisema  kesi za wadaiwa sugu wa kodi ya ardhi 736 zilizosikilizwa na baraza la ardhi la nyumba na wilaya Machi 12 mwaka huu  kwani  amri ya mahakama iliwataka wananchi kulipa madeni yao.

“Tangu kipindi cha kesi hizo mpaka hivi sasa viwanja vilivyopelekwa mahakamani vya jijini  na manispaa ya Ilemela tufalikiwa kukusanya sh Milioni 900 tofauti na matarajio ya idadi ya wananchi wanaodaiwa kwani amri ya mahakama imewataka wamiliki hao walipe kodi kwa kipindi cha siku kumi na nne na muda huo umepita na kuna baadhi yao hawajalipa.

“Kampuni ya madalali wa Rock City Tackers ya mkoani hapa imepewa jukumu la kufuatilia mali za wadaiwa sugu na itaanza rasmi  kazi ya kukamata mali hizo ili kuhakikisha madeni ya serikali yanalipwa kwani Mei 7 mwaka huu tutauza kwa njia ya munada viwanja  vya viwanda vinne vilivyopo kwenye halmashauri ya Magu kwani amri wazilizotolewa zimehusisha viwanja vyote vilivyopelekwa mahakamani,” alisema Kamihanda.

Hata hivyo amewataka wananchi waliofikishwa mahakamani ambao walipewa amri ya kulipa kodi hiyo na hawajatekeleza agizo hilo wanapaswa kutambua dalali ameanza kutekeleza rasmi  wajibu huo ambapo jumla ya viwanja 421 vitauzwa kwa amri ya mahakama kwa sababu  ya wamiliki kushindwa kulipa  madeni yao.

“Wamiliki hao waliofikishwa mahakamani ni wadaiwa sugu kwani  wamekaa muda mrefu na madeni hayo wapo  wenye madeni ya miaka mitano, sita hadi kumi kwa mujibu wa sheria ya ardhi inampelekea kuwa mdaiwa sugu wa kodi hii kwa sababu anatakiwa kila mwaka wa fedha anatakiwa kutimiza wajibu huo,”alisema Kamihanda.

Kamihanda  amewakumbusha wamiliki wa ardhi kulipa  kodi  kwa mujibu wa sheria ili kuepuka usumbufu unaojitokeza kiasi cha kupelekea hatua za kisheria kuchukuliwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,305FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles