26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Viwanja 186 Goba vimeingilia maeneo ya wazi

Na JONAS MUSHI -DAR ES SALAAM


unnamed-jpgnn

KAMPUNI binafsi ya upimaji ardhi ya Husea imebaini viwanja 186 kati ya 1,016 vilivyohakikiwa mipaka yake katika Mtaa wa Kunguru, Kata ya Goba Wilaya ya Ubungo, viliingilia maeneo ya wazi, hifadhi ya barabara na mito.

Hayo yalibainishwa juzi jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Husea, Renny Chiwa, wakati akiwasilisha mbele ya wakazi wa Kunguru taarifa na ramani ya awali ya mipaka ya baadhi ya viwanja vya mtaa huo.

Akizungumza na wananchi hao, alisema sheria inawabana kutopima viwanja hivyo hadi pale wamiliki watakapokubali kuacha sehemu za viwanja zilizoingilia maeneo yasiyotakiwa kujenga makazi.

“Wale wakazi ambao viwanja vyao vimeingia kwenye hifadhi za barabara na moto au maeneo ya wazi hatutaweza kuvipima na kuviwekea mawe ya mipaka hadi kuwepo kwa maridhiano ya kuachia sehemu hizo,” alisema Chiwa, ambaye pia ni Mtaalamu wa Mipango Miji aliyesajiliwa na Bodi.

Alisema kati ya viwanja 1,016 ambavyo mipaka yake imepitiwa, 801 vimeshajengwa, huku 215 vikiwa havijaendelezwa na kati ya hivyo, viwanja 830 ndivyo vyenye sifa ya kupimwa.

Alitoa wito kwa wananchi ambao hawajajitokeza kuorodhesha majina yao ili mipaka ya viwanja vyao iweze kupitiwa katika mradi huo wa upimaji ardhi kwa pamoja ambao unapunguza gharama za upimaji.

Akizungumza na MTANZANIA, Christopher Mayaheka, Mkazi wa Mtaa wa Kunguru, alisema elimu inahitajika kutolewa ili wananchi waweze kuitikia wito wa kupima ardhi kwa pamoja, kwani ni gharama nafuu.

Naye Mtendaji wa Mtaa wa Kunguru, Mohamed Kumbwani, aliliambia MTANZANIA kuwa zamani watu walikuwa wanatapeliwa katika upimaji ardhi, lakini sasa hivi Serikali imeamua kushirikiana na kampuni binafsi ambazo ziliwekwa wazi na Waziri mwenye dhamana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles