27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

VITURUBISHO VYA VYAKULA NJIA MBADALA KUONDOA SUMU MWILINI

Na Mwandishi Wetu,

ASILIMIA 80 hadi 90 ya magonjwa katika mwili wa binadamu husababishwa na sumu (Free Radicals).

Free radicals ni kemikali ambazo husababisha magonjwa sugu kama vile saratani na magonjwa ya moyo.

Mtaalam wa afya ya jamii na mkufunzi wa maisha kutoka Kampuni ya Trevo, Dk. Janeth Massawe anaelezea namna Free Radicals inavyosababisha magonjwa mbalimbali mwilini na njia bora za kuondoa free radicals. 

Dk. Janeth anasema sumu katika mwili wa binadamu hupatikana wakati mwili unapotengeneza nishati yake kwa kutumia Oxygen.

Anafafanua kuwa sumu au Free radicals ni muhimu katika miili kwa sababu zinapambana na magonjwa ambukizi mbalimbali yanayotokana na bakteria, fangasi na vimelea.

Pia kwa upande mwingine sumu ya mwilini ni hatari endapo zikizalishwa kwa wingi  kulingana na uhitaji wa mwili.

Anafafanua kuwa sumu ikizalishwa mwilini zinadhibitiwa na virutubisho vinavyotokana na vyakula tunavyokula ambavyo vinaitwa ‘antioxidants nutrients’.

“Sasa kama uzalishaji wa free radicals ni mkubwa kuliko kiwango sahihi kinachohitajika kwenye mwili, mwili ndio unaanza kupata maradhi mbalimbali.

“Kwa mfano kama ni kwenye mishipa ya damu mtu atapata matatizo ya moyo au kwenye tumbo atapata vidonda vya tumbo,” anasema  Dk. Janeth.

Anasema kama ni kwenye ngozi mtu anapata saratani ya ngozi au kunyauka kwa ngozi na maradhi mengine mengi ambayo hutegemea na sehemu ya mwili ambayo sumu zimezidi kiwango.

Kwa uhalisia kuna vitu vilivyotajwa hapo juu ambavyo ni rahisi kuepuka lakini kuna vingine ni vigumu kuepukika kama vyakula, kupigwa na mionzi ya jua kutokana na changamoto mbalimbali za maisha.

Watu wengi siku hizi wanahangaika kutafuta tiba na matibabu ya kuweza kupambana au kuondoa free radicals hizi mwilini ambapo hutumia dawa mbalimbali katika kupunguza tatizo hili.

Dk. Janeth anasema tiba nzuri kuliko zote ni viturubisho vya vyakula mbalimbali ambavyo ni salama zaidi.

Anafafanua kuwa kuna viturubisho vinavyopatikana katika kinywaji cha Trevo ambacho kimetengezwa kwa mimea, matunda, mbogamboga na mizizi ya asili.

“Trevo ni kirutubisho cha mwili cha kipekee ambacho hakijapata mshindani wa kulingana nacho hadi sasa,” anasema.

Ni mchanganyiko uliobuniwa na kufanikiwa kwa kiwango cha juu kurudisha, kukarabati na kuamsha afya ya mtu iliyodorora.

“Mchanganyiko huu hufanya kazi kwa kuupa mwili virutubisho vyote ambavyo umekosa kutokana na kula chakula cha kisasa kinachokosa virutubisho muhimu,” anafafanua.

Anasema ni mchanganyiko unaofanya kazi vizuri kwa mtu wa umri wa wote kuanzia mtoto wa miaka miwili hadi mtu mzima kwa muda mfupi.

Kwa mujibu wa mtaalamu huyo anasema Trevo inauwezo wa kupambana na free radicals zisizopungua 400,000.

“Binadamu wa kawaida anapaswa apate angalau virutubisho 90 vyenye uwezo wa kupambana na free radicals wasiopungua 7,000 (orac rate),” anasema.

Hivyo, mtu anayetumia viturubisho vya Trevo anakuwa kwenye nafasi nzuri kiafya kwani anapitiliza kwa kupata 13,000 orac rate kwa siku.

Anaelezea kuwa hata mtu ambaye anakula milo yote vizuri, ukweli ni kwamba hakuna mwanadamu anayeweza kufikisha mahitaji  hayo ya mwili kwa sababu mwili hauna uwezo wa kufyonza virutubisho vyote vinavyotokana na vyakula tunavyokula.

“Faida kubwa ya kiturubisho cha Trevo ni kuwa na chembechembe ndogondogo hivyo mtu akitumia  inaenda moja kwa moja kwenye mfumo wa damu hakuna kinachopotea,”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles