‘Vituo vya masoko ya madini vimeongeza mapato’

0
748

Amina Omari, Tanga

Serikali imesema kuwa uanzishwaji wa vituo vya masoko ya madini nchini umesaidia kuongeza makusanyo ya mapato.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Madini, Doto Biteko wakati akifungua mkutano mkuu wa nane wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji nchini (FEMATA), uliofanyika mkoani Tanga.

Akitolea mfano wa Mkoa wa Mara amesema ndani ya mwezi mmoja wameweza kukusanya kutoka kiasi cha Sh milioni 142 hadi kufikia Sh milioni 475 za madini ya dhahabu.

“Wakati tunaanzisha vituo hivi kuna wajanja wachache walianza kutuhujumu lakini tuliweza kuwadhibiti na tunaendelea kuwadhibiti,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here