24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

VITUO 23 VYA REDIO VYAFUNGIWA UGANDA

KAMPALA, UGANDA


TUME ya Mawasiliano Uganda (UCC), imefungia vituo 23 vya redio vya FM kwa madai ya kutangaza ‘uganga wa kienyeji na kuwatapeli wananchi.’

Tangazo hilo la kufungiwa vituo hivyo, limetolewa juzi jioni na mwenyekiti wa UCC, Godfrey Mutabazi.

Mutabazi ameshutumu redio hizo kutumiwa na waganga kuwatapeli wananchi na kuvunja sheria ya uchawi ya kifungu cha pili.

Redio hizo zimekuwa zikitoa vipindi kwa waganga kutangaza shughuli zao huku wakiwaambia wananchi kutuma fedha kupitia simu za mikononi.

Msemaji wa UCC, Pamela Ankunda amesema kuwa, “Kwa kuwaweka hewani matapeli wanaojiita waganga wa kinyeji, wakitumia mbinu mbali mbali wakiwa hewani ili kuwatapeli wananchi.”

“Kwa mfano kwa kuwalaghia wananchi kuwa ukituma fedha kwa njia ya simu ya mkononi utapata utajiri, kesho yake utapata mamilioni ya fedha chini ya kitanda chako. Hivyo tumetumia sheria ya kuziwajibisha radio hizo baada ya kusikiliza matangazo hayo,” alisema Ankunda

Tume imewataka wamiliki wa redio zote zilizofungiwa kufika ofisini, ikisema vituo hivyo vina nafasi ya kufunguliwa vikifuata sheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles