30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

VITU VILIVYOPEWA JINA LA OBAMA ILI KUMUENZI

shule

Na MWANDISHI WETU,

BARACK Obama amestaafu nchini Marekani akiwa ameacha vitu kama maktaba, barabara na shule vikiwa vimepewa jina lake ikiwa ni ishara ya heshima aliyopewa na Wamarekani.

Kutakuwa na Maktaba ya Rais Barack Obama mjini Chicago. Pia kuna shule nyingi zilizopewa jina la kiongozi huyo wa kwanza Mwamerika Mweusi nchini humo.

Mbali na hayo, kuna vitu vingi ambavyo huwezi kutarajia vilivyopewa jina lake ikiwamo vimelea na buibui.

 Kimelea

Kuna mnyoo aina ya Baracktrema obamai, ambao umepewa jina la Rais Barack Obama

Mnyoo huo ambao kisayansi huitwa Baracktrema obamai ni kimelea cha pili kupewa jina la Obama.

Mnyoo huu ni mrefu na unafanana na uzi, huambukiza kasa wa maji yasiyo na chumvi Malaysia na unaweza kuua.

“Hili ni jambo jema bila shaka, tumefanya hivi kwa heshima ya rais wetu mstaafu,” anasema Dk. Thomas R Platt, ambaye ni mtaalamu wa vimelea wa kasa na mgunduzi wa aina hiyo ya mnyoo.

Mbali na mnyoo huo, watafiti waliwahi kuupa mnyoo unaopatikana nchini Kenya jina la Paragordius obamai, ambao uligunduliwa karibu na nyumbani kwa Obama.

Samaki

Samaki anayepatikana katika hifadhi ya viumbe wa baharini ya Papahanaumokuakea.

Ikiwa ni sehemu ya kutoa heshima kwa Obama kwa juhudi zake za uhifadhi wa viumbe wa baharini katika Bahari ya Pasifiki. Wanasayansi walimpa samaki mmoja anayepatikana eneo la Kure Atoll katika hifadhi ya Papahānaumokuākea, pwani ya Hawaii jina la rais huyo. Samaki huyo ana rangi ya damu ya mzee na dhahabu.

Mwaka 2012, watafiti walimpa jina Etheostoma Obama samaki mwingine wa rangi ya samawati na manjano. Samaki huyo hupatikana katika mito ya Duck na Buffalo inayotoa maji yake kutoka kwa Mto Tennessee.

 Mjusi

Mjusi mwenye urefu wa futi moja na aliyekuwa na meno yaliyosimama wima alipewa jina la Obamadon kutokana na tabasamu la Obama.

Mlima

Obama ni miongoni mwa marais wa Marekani ambao wana milima iliyopewa majina yao. Taifa la Antigua lilibadili jina la mlima mrefu zaidi nchini humo, mlima wa Boggy kuwa Mlima Obama.

 Kuvu

Mwaka 2007, watafiti walizipa kuvu (ukungu wa miti na miamba) jina Caloplaca obamae, pindi Obama alipoanza kufanya kampeni yake ya urais. Walichukua hatua hiyo kwa sababu ya Obama kuunga mkono masomo ya sayansi.

 Kituo cha mafuta

Kijiji cha Moneygall katika eneo la Offaly, katikati mwa Dublin na Limerick nchini Ireland, kuna kituo cha mafuta ambacho kilipewa jina la Obama.

Katika Barack Obama Plaza kuna kituo cha mafuta, mgahawa na kituo cha wageni ambacho hutoa habari kuhusu uhusiano wa Obama na Moneygall.

Kijiji cha Moneygall ndicho asili ya babake babu wa babu wa Rais Barack Obama.

 Mkate

Kabla ya Rais Obama kuzuru Ireland, waokaji wa mikate walikimbia kuoka mikate maalumu.

Mkazi wa Moneygall, Joseph Kearney aliwasilisha mikate maalumu kwa majamaa wa Obama nchini Ireland waliokuwa wakijiandaa kwa ziara yake.

Haijulikani iwapo Obama alikula mikate hiyo au la.

 Ndege

Kuna ndege anayepatikana Amazon magharibi ambaye amepewa jina Nystalus obamai.

 Shule Kenya

Katika kijiji cha Kogelo, alikozaliwa baba yake Obama, kuna shule mbili, Shule ya Msingi Senator Obama Kogelo na Shule ya Sekondari Senator Obama Kogelo.

Zilipewa majina hayo Obama alipokuwa seneta wa Illinois.

 Buibui

Kuna buibui anaitwa Aptostichus barackobamai wa aina ya trapdoor, ambao wamepewa jina hilo kutokana na Obama kuwa shabiki wa Spider-Man.

Wengine huitwa Aptostichus stephencolberti (kutokana na mchekeshaji Stephen Colbert) na Aptostichus angelinajolieae (kutokana na mwigizaji Angelina Jolie).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles