29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 20, 2021

VITA YA LIGI KUU YAAMIA FA

Na ZAINAB IDDY


NI msimu mwingine wa Kombe la Shirikisho, na nusu fainali nyingine yenye upinzani wa hali ya juu baina ya timu nne za Ligi Kuu Tanzania Bara zilizofanikiwa kuvuka vizingiti hadi kufikia hatua hiyo.

Michuano hiyo imeendelea kwa mara ya pili, ambapo msimu uliopita Yanga ndio waliofanikiwa kutinga fainali na kunyakua taji hilo kwa kuifunga Azam kwa penalti.

Kabla ya Yanga na Azam kuvaana fainali, nusu fainali yenyewe ilizikutanisha timu ambazo zote hazikutaka kuruhusu makosa yoyote yatakayowafanya washindwe kufika fainali; Mwadui dhidi ya Azam, Coastal wakiikaribisha Yanga mkoani Tanga.

Ukweli ni kwamba upinzani ulikuwa wa hali ya juu, Azam wakipata ushindi wao kwa penalti baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 ndani ya dakika 90. Huku Yanga wao wakipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union, lakini mchezo huo uligubikwa na matukio yenye utata yaliyopelekea timu hiyo ya Tanga kutozwa faini.

Kama kanuni za mashindano hayo zinavyotaka, jumla ya timu 64 zimeshiriki msimu huu ambapo timu 16 zilitoka Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL), timu 24 ligi daraja la kwanza na timu 24 kutoka ligi daraja la pili.

Baada ya kuchezwa kwa raundi ya kwanza, timu 16 hupatikana kutoka ligi kuu na nyingine kwa idadi hiyo hiyo zikitoka kwenye ligi hizo za chini, ambapo sasa zitakutana kwenye raundi ya pili kabla ya kutinga hatua ya robo fainali, nusu na fainali yenyewe ya mashindano hayo ambayo bingwa wake atanyakua kitita cha milioni 50 za Kitanzania.

Aidha, mshindi wa michuano hiyo atapata nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF) mwakani.

Mashindano ya mwaka huu ni Simba, Yanga na Azam pekee zimeonekana kuwa wababe zaidi tofauti na timu nyingine zilizoshiriki mwaka jana baada ya kutinga hatu ya nusu fainali kwa mara nyingine ingawa Mbao FC nao wameonesha uwezo wao hadi kufikia nusu fainali, na swali lililopo ni je, watasonga mbele zaidi ya hapo?

Upinzani ulionyesha katika Ligi Kuu Tanzania Bara hadi sasa unaonekana kuhamia FA baada ya kila mmoja kati ya zilizotinga nusu fainali kuhitaji kutwaa kombe hilo lakini pia zilionekana zinavita kubwa pale zilipokutana VPL.

Yanga

Ndio walioitimisha timu nne zilizoingia nusu fainali mwaka huu katika mashindano hayo baada ya kuondoa Tanzania Prisons kwa mabao 3-0, mechi iliyochezwa Jumamosi iliyopita Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Licha ya Yanga kuhitaji kutetea taji lake la Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu lakini pia, anahitaji kubaki  pia na lile la FA alilolichukua mwaka jana kwa kuichapa Azam.

Ni wazi Yanga watakutana na changamoto kutoka kwa Simba na Azam, kama ilvyoonekana katika siku za hivi karibuni, lakini pia uwepo wa Mbao nao ni wa kuchungwa kutokana na ukomavu wanaoupata kwenye ligi msimu huu.

Azam FC

Wanalambalamba hao waliingia hatua hiyo baada ya kuwatoa Ndanda FC kwa kuifunga mabao 3-1 kwenye mchezo wa robo fainali uliochezwa Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.

Washiriki hao wa fainali ya msimu uliopita, Azam, imetinga nusu fainali kwa mara ya pili tangu michuano hiyo ilipoanzishwa mwaka jana, wakionesha wazi kupania kulipata kombe hilo baada ya kulikosa lile la Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Rekodi zinaonyesha kuwa Azam amekuwa akizisumbua sana timu za Simba na Yanga kila wanapokutana, ingawa pia nayo imeonekana kutoka kapa mbele ya Mbao FC hivyo yoyote kati ya hizo ikipangwa naye hatua ya nusu fainali au fainali, ni wazi kutakuwa na upinzani mkali ndani ya uwanja.

Simba

Kwa mara ya kwanza mwaka huu wameweza kufika hatua hiyo baada ya mwaka jana kujikuta wakiondolewa na Coastal Union kwa kichapo cha mabao 2-1.

Kuingia kwenye hatua hiyo kunaongeza hali ya kulisaka taji mwaka huu, kutokana na ukweli kuwa kwenye ligi bado hajajulikana bingwa, hasa baada ya Simba na Yanga zinazowania ubingwa kupishana kwa pointi chache, hivyo iwapo kama atalipata taji la FA atapata nafasi ya kushiriki Kombe la Shirikisho mwakani.

Mbali na hilo Simba huenda wakawa na uhitaji mkubwa zaidi wa kushiriki mashindano ya kimataifa ikiwa ni baada ya kukosa nafasi hiyo kwa misimu minne sasa, lakini pia upinzani wake mbele ya timu za Yanga, Azam na Mbao huenda ukawa kikwazo cha kufikia lengo lao hilo.  

Mbao FC

Ndio waliokuwa wa kwanza kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kuifunga Kagera Sugar kwa mabao 2-1, mechi iliyochezwa Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera.

Mbao imeingia katika hatua hiyo muhimu huku ikiwa na lengo moja pekee la kuhakikisha inatinga fainali kwa gharama yoyote ukizingatia pia timu hiyo iliyopanda daraja na kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu imeweza kuonyesha ushindani wa hali ya juu kwa vigogo wa soka Simba, Yanga na Azam FC.

Mchezo huo ulianza kwa kasi kila timu ikijaribu kufanya mashambulizi lakini Azam FC ndio waliofanikiwa kupata bao dakika ya 13, lililofungwa na Shaaban Idd baada ya kumzidi maarifa kipa wa Ndanda, Jeremiah Kisubi.

Baada ya bao hilo Ndanda walicharuka na kusawazisha likifungwa na William Lucian, dakika ya 14 aliyepiga shuti la moja kwa moja baada ya kipa wa Azam FC, Aishi Manula, kuokoa kwa ngumi mpira uliokuwa unaelekea golini kabla ya kumponyoka na kumfikia mfungaji aliyeunganisha wavuni.

Azam FC walipata bao la pili lililofungwa tena na Idd, dakika ya 44 baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Ndanda na kuubetua mpira uliompita kipa na kuingia golini na kufanya Azam FC iende mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-1 Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Ramadha Singano akaifungia Azam bao la tatu baada ya kupiga krosi iliyojaa moja kwa moja wavuni.

Hiyo ilikuwa ni mechi ya robo fainali ya tatu, ikiwa imesalia robo fainali moja kati ya Yanga na Prisons zinazotarajiwa kuchezwa Aprili 22 mwaka huu. Bingwa wa michuano hiyo anaiwakilisha nchi kwenye michuano ya kombe la Shirikisho Afrika.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,594FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles