25.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Virusi vya Zika kuambukiza watu bilioni mbili Afrika

Original Title: Aa_FC3_58a.jpg

LONDON, UINGEREZA

WATU zaidi ya bilioni mbili wanaweza kuwa katika hatari ya mlipuko wa virusi vya Zika katika baadhi ya maeneo ya Afrika na Asia, kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa Kwenye jarida la masuala ya kitabibu la Lancet.

Wakazi wa nchi za India, Indonesia na Nigeria ni baadhi ya wale walio katika hatari ya kupata maambukizi ya virusi vya Zika, utafiti umesema.

Walifanyia kazi taarifa za watu wanaotumia usafiri wa ndege kufanya utafiti wao huo.

Hata hivyo, wamebainisha kwamba, kinga kwa virusi hivyo inaweza kuwepo katika baadhi ya maeneo na hivyo kuweza kupunguza uwezekano wa hatari.

Jopo la watafiti kutoka Chuo cha Masuala ya Usafi na Tiba ya Magonjwa ya Maeneo yenye Joto cha London, Chuo Kikuu cha Oxford na kile cha Toronto, nchini Canada, linasema ‘ Watu wa wengi  ni miongoni mwa wanaoishi katika mazingira ambayo itakuwa vigumu kuzuia, kubaini na kushughulikia virusi vya Zika.

Waliangalia masuala kama vile idadi ya watu wanaosafiri kutoka maeneo yaliyoathiriwa na Zika ya Amerika ya Kusini kuelekea Afrika na Asia.

Aidha walipitia uwezo wa mbu, ambao wanaweza kusafirisha virusi na hali ya hewa katika kanda hizo katika kutathmini ni nchi gani inayoweza kuwa na hatari ya mlipuko huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles