25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Virusi vya Corona vyaua wawili Iran

TEHRAN, IRAN

IRAN  imethibitisha vifo vya watu wawili vilivyotokana na maambukizi mapya ya virusi vya Corona na hivyo kuwa vifo vya kwanza kuripotiwa eneo la Mashariki ya Kati.

Nchini China maambukizi yanaendelea kupungua ingawa wataalamu wanaonya kwamba virusi hivyo vinaweza kuenea zaidi kuliko ilivyodhaniwa. 

Maofisa wa afya nchini Iran, walithibitisha visa viwili vya maambukizi mapya ya virusi vya Corona vilivyopewa jina la COVID-19 ambapo wanaume wawili wazee wamepoteza maisha katika mji wa Qom. 

Shirika la habari la Iran, IRNA, limesema shule na vyuo huenda vikafungwa katika mji huo wa Qom kwa ajili ya kufanya uchunguzi.

Iran imeanza kuchukua hatua za tahadhari hususan katika viwanja vya ndege ambapo abiria tofauti wanawasili. 

Vifo hivyo ni vya kwanza kuripotiwa katika eneo la Mashariki ya kati. 

Wakati huo huo maambukizi ya Corona yameripotiwa katika nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu.

Idadi ya vifo ndani ya China bara imefikia watu 2,118 baada ya watu wengine 114 kufariki, lakini maofisa wa afya wameelezea kiwango kidogo cha maambukizi mapya tofauti na hapo awali. 

Zaidi ya watu 74,000 wameambukizwa virusi hivyo ndani ya China na mamia wengine katika nchi zaidi ya 25.

Wakati China ikishuhudia kupungua kwa maambukizi ya mripuko wa COVID-19, Serikali ya Japan inakabiliwa na ukosoaji mkubwa juu ya hatua za kuiweka chini ya karantini meli ya Diamond Princess. 

Michael Ryan ambaye ni Mkurugenzi wa huduma za dharura kutoka WHO na anasema;

“Ni dhahiri kwamba mamlaka za Japan awali zilifanya uamuzi wa kuwaweka karantini abiria wote kwenye meli hiyo, ambapo abiria waliwekwa pamoja katika mazingira ambayo wanaweza kufuatiliwa na kupatiwa makazi tofauti na kila kitu kingine”.

Juzi  Jumatano karibu abiria 500 waliondolewa ndani ya meli hiyo baada ya kubainika kutokuwa na maambuki ya corona. 

Abiria zaidi waliondoka ndani ya meli hiyo jana Alhamis.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles