24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Virusi vya corona vyasababisha Papa kuongoza ibada kwa njia ya video

ROME, ITALIA

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis hataonekana hadharani ili kuzuia kukutana na mikusanyiko ya watu inayofika kumwona.

Hatua hiyo imekuja wakati maambukizi na vifo vilivyotokana na virusi vya corona nchini Italia vikiwa juu kuliko nchi nyingine yeyote duniani baada ya China.

Inaelezwa kuwa kwa sasa kiongozi huyo wa kiroho ataendesha shughuli zake nyingi  ikiwa ni pamoja na kuongoza ibada kwa njia ya video kupitia mtandao wa intaneti.

Shughuli hiyo ataifanya  kutoka ndani ya  Vatican kwa sababu ya maambukizi ya virusi vya corona nchini Italia.

Vatican pia imesema kuwa Papa hatatumia utaratibu wa kuzungumza na mkusanyiko wa watu kupitia dirisha  linalotazama kanisa la Mtakatifu Petro mjini Roma  ambalo ni kubwa kuliko yote duniani.

Zaidi  hatakuwa na mikutano mingine katika eneo hilo  au siku ya Jumatano.

Papa mwenye umri wa miaka 83 hajafanya  misa hiyo ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi chote cha upapa wake.  

Pamoja na hayo  Vatican inasema kiongozi huyo anasumbuliwa tu na baridi ambayo haina dalili zinazohusiana na magonjwa mengine.

Wakati kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki Duniani, akichukua uamuzi huo, idadi ya watu  waliokufa kwa virusi vya corona nchini Italia imepanda hadi kufikia 197  baada ya ongezeka la vifo vingi kila siku tangu maambukizi hayo yazuke.

Maofisa wanasema watu 49  wamekufa nchini humo ndani ya saa 24, wakati kukiwa na maambukizi ya zaidi ya kesi 4,600 zilizoripotiwa.

Nchi hiyo sasa imeripoti vifo vingi nje ya China, ambako virusi hivyo vilizuka mwezi Desemba katika mji wake wa Wuhan ulioko  katika jimbo la Hubei.

Shirika la Afya Duniani la (WHO) linasema karibu watu 100,000 duniani kote wameambukizwa virusi hivyo huku zaidi ya 3,000 wakifa wengi wao wakiwa ni kutoka China.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles