25.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Virusi vya Corona: New York yarekodi wagonjwa wengi zaidi duniani

NEW YORK, MAREKANI

JIMBO la New York, sasa lina visa vingi vya virusi vya corona zaidi ya taifa lolote duniani , kulingana na takwimu mpya.

Serikali imethibitisha kwamba idadi ya visa vya ugonjwa huo imeongezeka kutoka 10,000 siku ya Alhamisi hadi 159, 937 na kuiweka mbele ya Uhispania iliyo na visa 153,000 na Italia iliyo na visa 143,000.

China ambapo virusi hivyo vilianza mwaka uliopita iliripoti visa 82,000.

Marekani yote imerekodi visa 462,000 na takriban vifo 16,500.

Kote duniani kuna takriban visa milioni 1.6 na vifo 95,000.

Huku Jimbo la New York likiongoza ulimwengu katika visa vya maambukizi , takriban watu 7000 wamefariki katika mji huo, ikiwa nyuma ya Uhispania iliyo na vifo 15,500 na Italia iliyo na 18,000 ikiwa ni mara mbili ya vifo vya China 3,300.

Takriban majeneza 40 yalizikwa siku ya Alhamisi katika kaburi la pamoja jijini New York.

Picha zilizochukuliwa na kamera za juu zilionyesha wafanyakazi wakitumia ngazi kuingia katika kaburi hilo kubwa ambapo majeneza hayo yalikuwa yamewekwa.

Picha hizo zilichukuliwa katika eneo la Hart Island kando ya mji wa Bronx , ambao umekuwa ukitumika kwa zaidi ya miaka 150 na maofisa wa baraza la mji kama eneo la makaburi ya pamoja kwa wale wasio na familia na wasioweza kumudu mazishi.

Operesheni za mazishi katika eneo hilo zimeongezeka kutokana na mlipuko wa virusi kutoka siku moja kwa wiki hadi siku tano kwa juma, kulingana na Idara magereza.

Wafungwa kutoka kisiwa cha Rikers ndio ambao wamekuwa wakifanyakazi hiyo, lakini ongezeko la kazi limefanya kazi hiyo kuchukuliwa na wanakandarasi.

Meya wa mji wa New York, Bill De Blasio amesema mapema wiki hii kwamba maziko ya umma ya mji huo huenda yakatumika wakati wa mlipuko huu.

“Ukweli ni kwamba tumetumia Kisiwa cha hart kwa muda mrefu,” alisema.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,522FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles