30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

‘VIROBA’ KUATHIRI MAELFU YA AJIRA

AGIZO la Serikali kupiga marufuku matumizi ya pombe kali za kwenye mifuko ya plastiki maarufu ‘viroba’, linatarajiwa kuathiri maelfu ya ajira za watu waliokuwa wakijipatia kipato kupitia kinywaji hicho.

Kaimu Meneja Mkuu wa  Tanzania Distilleries Limited (TDL), ambayo ni kampuni tanzu ya TBL Group, Devis Deogratius amesema kampuni hiyo imeajiri zaidi ya watu 200 na wengine zaidi ya 360 wakiwa ni vibarua na ajira nyingine zisizo rasmi kupitia baa mbalimbali nchi nzima pamoja na wasambazaji wa jumla na rejareja wanaofaidika na viroba.

Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage amesema viwanda pamoja na wazalishaji wa pombe za ‘viroba’ wanatakiwa kufuata maagizo ya Serikali kuhusiana na uzalishaji wa pombe hiyo.

“Kama kuna mzalishaji anayedhani kuna jambo lolote halipo sawa kwenye agizo hilo, awasilishe malalamiko yake Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira,” amesema Mwijage.

Aidha baadhi ya wafanyabiashara wa vileo katika jiji la Arusha wamelalamikia uamuzi wa Serikali kupiga marufuku uuzaji wa ‘viroba’ kwa madai kuwa muda wa Februari Mosi uliotolewa kuviondoa viroba hivyo sokoni ni mfupi mno.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles