30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Vipodozi feki, vyakula vyakamatwa Songea

Na AMON MTEGA-SONGEA

IDARA ya Afya katika Manispaa ya Songea, Mkoa wa Ruvuma, imefanikiwa kukamata vipodozi na vyakula vyenye sumu vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni mbili.

Taarifa hiyo ilitolewa jana na Ofisa Habari, Manispaa ya Songea, Albano Midelo, alipokuwa akizungumza na MTANZANIA ofisini kwake.

Kwa mujibu wa Midelo, vipodozi na vyakula hivyo, vilikamatwa katika kipindi cha kuanzia Aprili hadi Juni, mwaka huu, kupitia ukaguzi endelevu unaofanywa na idara hiyo.

Alivitaja baadhi ya vipodozi hivyo alivyosema vina sumu kuwa actif plus, betasol, broze, cocoderm, carolight, carotone, citrolight, clairmen, cocopulp, corton, dipLoson na epiderm.

Vingine ni extralair, jaribu, lemonvate, mekako, miki, montclair, movate, naomi, oranvategel, perfect, princes, rapid, sabuniprotex, sevenmirackes, toplemon, whiteplus, dodo, teint, superclair, greeting, 14days, dermotyl, natural, goldtouch, cocodermbetacort, extralwhite, fomura avas, lemon cream na diva maxmum.

“Pamoja na kuvikamata vipodozi hivyo, pia tulikamata vipodozi halali vilivyomaliza muda wake wa matumizi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi laki tano.

“Vipodozi hivyo ni pamoja na skin soft, pure glycerine, royal touch, u&me na mambo fresh.

“Kwa upande wa vyakula, tulikamata vile vilivyokwisha muda wake wa matumizi ambavyo vilikuwa na thamani ya zaidi ya shilingi laki tatu.

“Kwa hiyo, nawaomba wananchi na wafanyabiashara kwa ujumla, wawe makini na wasijihusishe na uuzaji wa bidhaa zisizoruhusiwa, wakikamatwa watachukuliwa hatua za kisheria,” alisema Midelo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles