24.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Vipaji tunavyoviibua ligi ya vijana tuviendeleze

LIGI Kikapu ya Vijana inayoshirikisha wanafunzi wa shule za sekondari, imekuwa msingi mzuri wa kuendeleza mchezo huo ambao umeonekana kusuasua hapa nchini

Ligi hiyo inayojulikana kama ‘Junior National Basket Association (JR.NBA)’, ilianza rasmi mwaka 2016 , na imekuwa ikifanyika kwenye Viwanja wa JMK Park jijini Dar es Salaam.

Baada ya kupata mafanikio makubwa mwaka wa kwanza tangu kuanzishwa kwake, mwaka 2017 ilishirikisha pia wasichana, lengo likiwa kuwajengea msingi bora na kukuza vipaji vya mchezo huo wenye umaarufu mkubwa nchini Marekani.

Kutokana na ligi hiyo kuchezwa kwa muda mrefu,ni dhahiri vijana wanaoshiriki wamejengwa na kujua misingi yote ya kikapu.

Kwa kawaida ligi hiyo huanzia katika hatua ya makundi huku wachezaji wakipata mafunzo mbalimbali ya mchezo hadi kufikia hatua ya mtoano na hatimaye fainali.

Ni jambo la kupongezwa kwa aliyetoa wazo la kuanzishwa kwa ligi hiyo , hasa kutokana na hali ya mchezo wa mpira wa kikapu ilivyo kwa sasa hapa nchini, kwani mvuto umepungua tofauti na miaka ya nyuma.

Ni wazi vipaji vingi vimeibuliwa, ni jukumu la wahusika wa sekta hiyo kuangalia kwa jicho la tatu wachezaji hao ili baadaye waweze kuliletea faida Taifa.

Ifahamike kwamba, kuzorota kwa mchezo huo ni matokeo ya kushindwa kuandaa wachezaji kuanzia ngazi za chini, hasa baada ya michezo ya shule kusimama kwa kipindi  kirefu.

Ni jukumu la Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) ambao ni wasimamizi wa mpira wa kikapu hapa nchini, kuvifuatilia vipaji  vilivyoibuliwa kwa jicho la tatu,  kwa kuwa  wakiendelezwa kuna uwezekano mkubwa wa kurudisha hadhi ya mchezo huo.

Tumeshuhudia Tanzania ikifanya vibaya katika michuano tofauti na hata kushindwa kushiriki baadhi ya mashindano kwa kukosa timu imara za kiushindani, hali hiyo inachangiwa kwa kiasi kikubwa na mfumo uliopo wa uendeshaji wa ligi ya mchezo huo.

Ligi za kikapu zinazoendeshwa bila kuzingatia umuhimu wa kuibua vipaji vipya, mara nyingi timu zinazoshiriki ni zile zile.

Bila kuwapo kwa utaratibu mzuri wa kuwaendeleza vijana ni wazi watavunjika moyo.

Nina imani kubwa vipaji vipya vinaweza kuleta mabadiliko katika mpira wa kikapu kwakua wengi wao wamepitia kwenye mafunzo bora yanaoendana na sheria za sasa za mchezo huo.

Baadhi ya wachezaji maarufu wa NBA, Marekani, wamekuwa wadau wakubwa katika kusapoti programu ya vijana hao,  hivyo ni lazima TBF nayo itoe kipaumbele zaidi ikiwamo kuzihimiza klabu kuwachukua na kuwatumia kwenye timu zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles