28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 23, 2021

VIONGOZI WAWEKA MSIMAMO UINGEREZA KUJIONDOA EU

BRUSSELS, UBELGIJI


VIONGOZI wa Umoja wa Ulaya (EU) wamekubaliana kwa kauli moja kuunga mkono mkakati madhubuti kuhusu Uingereza kujiondoa kutoka umoja huo.

Hayo yalifikiwa katika mkutano wa kilele wa viongozi wa nchi 27 wanachama wa umoja huo uliofanyika hapa juzi.

Viongozi hao walitaka Uingereza kuwa na msimamo thabiti kuhusu haki za raia wa EU kabla ya mazungumzo kuanza.

Katika ishara ya umoja miongoni mwao, viongozi hao walikubaliana kuhusu taratibu na muongozo utakaofuatwa katika mazungumzo ya kuelekea Uingereza kujiondoa rasmi EU.

Hata hivyo, Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May amezishutumu nchi hizo 27 wanachama EU kwa kukubaliana msimamo dhidi ya Uingereza.

Matamshi yake yalionekana kujibu mtizamo wa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kuwa Uingereza ina njozi tamu kuhusu mazungumzo hayo.

Merkel alisema hayo akimaanisha kuwa Uingereza isitarajie upendeleo au hadhi maalumu sawa na zile wanazopata wanachama, bali itachukuliwa kama mshirika tu.

Lakini pia kufuatia shutuma hizo za May, Merkel alisema hakuna njama za pamoja dhidi ya Uingereza bali msimamo wa umoja huo umelenga kulinda maslahi yake.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,900FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles