31.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

Viongozi wanne Chadema Kilolo wakimbilia CCM

Francis Godwin -Iringa

VIONGOZI wanne wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kata ya Ihimbo, Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa, wamefunga ofisi yao na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Wameeleza kujitoa Chadema wakidai kuridhishwa na utendaji kazi wa mkuu wa wilaya ya Kilolo, mbunge na diwani wao.

Viongozi hao, Katibu Kata, Livingiston Chang’a ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Halmashauri ya Kijiji cha Utengule, Mwenyekiti  wa Kata ya Ihimbo, Baton Ndenga, aliyekuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Utengule, Pangarasi Mkakatatu na Mwenyekiti wa Kitongoji  cha Magangamatitu, Jordan Mkakatu walikabidhi kadi za Chadema kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya  Wazazi CCM, Erasto Sima jana.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi ya CCM, Chang’a alisema awali walikuwa wanachama wa chama hicho kabla ya kujiunga upinzani.

Alisema walilazimika kwenda upinzani ili kuwapigania wananchi, lakini tangu wamekuwapo huko hakuna hoja mpya.

Chang’a alisema tangu wamekuwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asia Abdallah, amekuwa akifika   kwenye kata yao kushiriki shughuli nyingi za maendeleo.

Alisema changamoto zilizokuwapo ambazo wao wakati wanajiunga na upinzani walikuwa wakizisemea, tayari zimefanyiwa kazi na Serikali.

Akiwashukuru wanachama hao, Mbunge wa Kilolo, Venance Mwamoto, aliwapongeza kwa kutambua kazi zinazofanywa na CCM katika kata yao.

Kwa upande wake, Sima alisema viongozi hao wameonyesha imani kubwa kwao.

“Binafsi nawapongeza viongozi wa Chadema ambao mmerejea  CCM, mmeonyesha imani kubwa kwa Serikali, karibuni,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles