24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

VIONGOZI WAASTAFU WAONGOZA MAZISHI YA KAHAMA

Na PATRICIA KIMELEMETA -DAR ES SALAAM


VIONGOZI wakuu wastaafu wameongoza mazishi ya waziri wa kwanza wa mambo ya ndani wa iliyokuwa Serikali ya Tanganyika, Sir George Kahama.

Kahama ambaye alifariki dunia mwishoni mwa wiki iliyopita kwa ugonjwa wa figo, alizikwa jana katika makaburi ya Kinondoni.

Viongozi hao ni pamoja na marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete ambao waliambatana na wake zao.

Wengine ni mawaziri wakuu wastaafu, Jaji Joseph Warioba, Dk. Salim Ahmed Salim, Cleopa Msuya, Frederick Sumaye na Edward Lowassa.

Walikuwapo pia Makamu wa Rais Mstaafu, Dk. Mohamed Gharib Bilali, Spika wa Bunge Mstaafu, Anne Makinda, Jaji Mkuu Mstaafu, Othman Chande, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, balozi mstaafu Job Lusinde na mawaziri wastaafu Bernad Membe, Ritha Mlaki na Basil Mramba.

 

MWINYI

Akizungumza kwa niaba ya marais wastaafu, Mzee Mwinyi alisema Watanzania wanapaswa kutenda mazuri ili wanapofariki waweze kusimuliwa kwa yale mazuri waliyoyaacha.

Alisema historia nzuri inamjenga mtu hata akifariki, waliobaki watamuadithia kulingana na uzuri wa historia yake kuliko kutenda mabaya.

Mzee Mwinyi alisema hali hiyo ndiyo iliyojitokeza kwa Sir Kahama ambaye alikuwa akitenda mazuri hadi sasa wananchi bado wanaadithia uzuri wa matendo yake, jambo ambalo linapaswa kuwa funzo kwa wengine.

“Ukitenda mazuri hata ukifa, waliobaki watakuadithia mazuri yako kwa sababu kuna kitu wamejifunza kutoka kwako, lakini ukitenda mabaya unaacha historia mbaya na kwamba watu watakusema kwa mabaya,” alisema.

 

JAJI WARIOBA

Naye Jaji Warioba, alisema alikutana na Sir Kahama wakati alipokuwa Shule ya Wavulana Tabora kipindi hicho akiwa na umri wa miaka 21, huku Sir George akiwa na umri wa miaka 31.

 

KINANA

Kwa upande wake, Kinana alisema vyama vya ushirika viliweza kutoa viongozi mbalimbali kuwa wapigania uhuru wa Tanganyika.

Alisema kuwa Kahama ni miongoni mwa viongozi aliyetoka kwenye chama cha ushirika cha Bukoba na kujikita kwenye shughuli za ukombozi wa taifa.

 

MBOWE

Kwa upande wake, Mbowe alisema Chadema inaungana na Watanzania wengine kuomboleza kifo cha Kahama.

Alisema mchango wake katika taifa ni mkubwa, jambo ambalo lilichangia kujenga nidhamu na uadilifu.

 

NAPE

Akitoa salamu za Serikali, Waziri wa Habari,  Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alisema Serikali inaungana na Watanzania wote kuomboleza msiba huo.

Alisema ni vigumu kuelezea historia ya Sir Kahama kwa sababu inajulikana kutokana na weledi na uadilifu aliokuwa nao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles