26.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 26, 2023

Contact us: [email protected]

Viongozi wa Olimpiki Kenya wakamatwa

Hassan Wario
Hassan Wario

NAIROBI, KENYA

MAOFISA watatu wa kamati ya Olimpiki nchini Kenya (Nock), wamekamatwa na polisi kwa madai ya matumizi mabaya ya uongozi wa timu hiyo jijini Rio de Janeiro, nchini Brazil.

Katibu mkuu wa Nock, Francis Paul, alikuwa wa kwanza kukamatwa na polisi katika kituo cha Muthaiga kilichopo Nairobi, huku viongozi wengine wawili, Stephen Arap Soi na James Chacha, wakikamatwa kwenye uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta.

Wawili hao walikamatwa walipowasili kutoka nchini Brazil, huku wakiwa na wanamichezo walioshiriki michuano ya Olimpiki.

Inadaiwa kuwa viongozi hao waliwaacha wanamichezo wao katika mazingira magumu mara baada ya kumalizika kwa michuano ya Olimpiki.

Serikali nchini humo iliamua kuivunja kamati hiyo ya Nock Alhamisi, huku Waziri wa michezo, Hassan Wario, akisema kuwa viongozi hao wamewafanya wanamichezo hao kushindwa kufanya vizuri kama walivyokusudia.

“Kuna viongozi ambao wanaweza kusababisha hali ya michezo nchini kuzidi kushuka, kwa kipindi cha hivi karibuni, tumekuwa tukituhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya, tulikosa tiketi za ndege kwa wanamichezo, hii yote ni kutokana na viongozi kuwa na mambo yao binafsi,” alisema Wario.

Hata hivyo, Kenya imefanya vizuri katika michuano hiyo ya Olimpiki baada ya kushinda medali sita za dhahabu, pamoja na sita za shaba, lakini Serikali haijaridhishwa na uongozi uliosimamia timu hiyo.

Kwa upande wa nchini Zimbabwe, Rais wa nchi hiyo, Robert Mugabe, aliwataka wanamichezo wote waliokwenda kushiriki michuano ya Olimpiki nchini Brazil, wakamatwe kutokana na kushindwa kufanya vizuri.

Zimbabwe walipeleka washiriki 31, lakini hakuna hata mmoja aliyerudi na medali, huku aliyefanya vizuri kati yao akishika nafasi ya nane.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,726FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles