29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Viongozi wa kijiji mbaroni kwa ramli chonganishi

NA  MURUGWA THOMAS

 WATU saba wakiwamo viongozi watatu wa Serikali ya Kijiji cha Ndevelwa katika Manispaa ya Tabora wanashikiliwa na   polisi kwa kushirikiana na waganga wa kienyeji kupiga ramli chonganishi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Emanuel Nley amesema viongozi hao walikamatwa Aprili 20 mwaka huu wakituhumiwa kuwaita na kuwahifadhi waganga hao wanne maarufu kwa jina la Lambalamba ama kamchape.

 Viongozi wanaoshikiliwa ni Rashid Ally (44) Mwenyekiti wa Kijiji cha Ndevelwa, Emanuel Jacob (68), Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mishagiwela na Ramadhan Juma (42) mwenyekiti wakamati ya shule ya msingi ya kijiji hicho.

 Kamanda Nley amewataja waganga wanaashikiliwa kuwa ni ndugu watatu, Omary Mohamed Nguyu (30),Taifa Omary  Nguyu(53) na Ramadhan Omary Nguyu (33) wakazi wa Kisarawe na mwenyeji wao, Juma Wengwa (43).

Alisema inadaiwa   Kamchape/ Lambalamba hao waliitwa na viongozi ili kwenda kutoa uchawi shuleni hapo kutokana na taarifa kwamba wanafunzi walikuwa wananguka darasani wakati wa masomo.

 Kukamatwa kwa Lambalamba hao kunafuataia taarifa zilizowafikia   polisi kwamba walikuwapo waganga wanne walioingia kijijini hapo kama kamchape ambao hufanya kazi za kutoa uchawi.

 Nley alisema waganga hao walikamatwa siku hiyo  asubuhi wakiwa na vifaa/zana mbalimbali ambazo hutumia kupigia ramli chonganishi vikiwamo vibuyu, shanga, nguo nyeusi, nyekundu na nyeupe   na mikia mitatu ( singa) ya wanyamapori ambao  haijafahamika.

 Kamanda Nley alisema uchunguzi wa tukio hilo  unaendelea kwa kushirikana na vyombo vingine na  utakapokamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles