28.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Viongozi wa dini waombwa kutoa elimu ya corona

Ashura Kazinja – Morogoro

VIONGOZI wa dini nchini wametakiwa kuhubiri na kusimamia mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa corona.

Rai hiyo imetolewa jana mjini hapa na Diwani wa Kata ya Mazimbu ambaye pia ni Meya wa Manispaa ya Morogoro,  Pascal Kihanga, wakati akigawa ndoo na sabuni za kunawa mikono katika misikiti na makanisa ya kata hiyo, na kuwataka viongozi hao kutaja kila mara neno la kujikinga na corona kwa waumini wao.

Kihanga alisema kuwa kila mtu anaabudu katika dini yake, hivyo vifaa hivyo vitasaidia katika mapambano hayo na kutoa wito kwa waumini kuvitumia pindi waingiapo na kutoka katika nyumba za ibada.

“Watu wengi siku ya Jumapili au Ijumaa wanaenda makanisani au misikitini, hivyo wachungaji na masheikhe wana wajibu wa kuwaelimisha waumini wao.

“Nimeamua kugawa ndoo mbili kila msikiti na kanisa katika kata yetu ili kuunga mkono jitihada za Serikali kupambana na ugonjwa wa corona,” alisema Kihanga.

Naye Mchungaji wa Kanisa la Barakuda, Jailos Maroda  aliahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika mapambano ya ugonjwa.

“Tumejisikia vizuri kukumbukwa wakati huu ambao tuko kwenye mapambano, ingawa tulikuwa tunaendelea na zoezi hilo, lakini kwa kuungwa mkono na viongozi wa Serikali imetutia nguvu zaidi na jambo jema sana,” alisema Mchungaji Maroda.

Imamu  wa Msikiti wa Aqswa, Sheikh Athuman Mussa, alisema kwa kutekeleza agizo la Serikali la kuwataka watu kunawa mikono kwa wingi iwezekanavyo, wamekuwa wakifanya hivyo sambamba na kutoa elimu kwa waumini wao kuhusu ugonjwa wa corona na namna ya kujinga.

“Hii kwetu sisi Waislamu sio jambo geni sana, kwani taratibu zetu na ustaarabu wetu hakuna anayefanya ibada bila kunawa mikono, miguu na uso, hivyo kwetu sisi ni mwendelezo, hivyo tukichanganya na hivi tulivyopewa vitasaidia zaidi,” alisema Sheikh Athumani.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles