31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Viongozi wa Dini nchini watakiwa kuendeleza Amani

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Viongozi wa Dini nchini wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuendeleza amani ya nchi na kusimamia maadili ya vijana ili kulinda Taifa na mmomonyoko wa maadili ambao umekuwa ukiongezeka siku hadi siku.

Akizungumza leo Juni 7, 2023 jijini Dar es Salaam Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila wakati wa mkutano wake na viongozi wa dini mbalimbali wakati akijitambulisha kwao amesema taasisi za kidini zinauwezo mkubwa kulinda maadili kwani zinaaminika na wananchi

Amesema katika uongozi wake atakuwa karibu na viongozi wa dini na kuwashirikisha katika mambo mbalimbali ya maendeleo pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zinazohusu taasisi hizo.

“Niwaombe viongozi mbalimbali na taasisi za Serikali kutatua changamoto zozote zinazohusu taasisi za dini kwani hizi ni muhimu sana mimi nikiamua kujitambulisha kwenu viongozi wa dini, kwani naamini katika Mungu na kazi zangu zote zinamtegemea Mungu,” amesema Chalamila.

Sambamba na hayo Chalamila amesema kuwa Serikali ya Mkoa huo ipo kwenye mchakato wa kulifanya soko la Kariakoo kufanyakazi kwa saa 24 ili kuendeleza na kukuza uchumi wa Taifa na mtu mmoja mmoja

“Tupo kwenye mchato huo hili soko letu lifanye kazi saa 24 kama magari yakiwa yanatembea usiku mtu anaweza kufika hapa saa 9 usiku akaenda kufanya manunuzi yake na akarudi kwenda kufanyabiashara zake,” ameongeza Chalamila.

Aidha, amewataka viongozi wa dini kuunda vikundi vya vijana waaminifu na wenye elimu ili kuweza kupatiwa mikopo na Serikali waweze kujikimu kimaisha.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Amani ambaye pia ni Kaimu Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Walid Alhad Omar amesema kuwa watashirikiana na mkuu wa mkoa kuhakikisha wanalinda na kuwajenga vijana kimaadili ambao ndio Taifa la kesho.

Upande wake, Shekhe Gullam Dewji amesema maadili yamemomonyoka kutoka na swala la uigaji wa malezi kutoka nchi nyingine nakuacha utamaduni wetu hivyo turejee kwenye utamaduni wetu wa malezi wa watoto ambao umekuwa ukusaidia malezi bora na maadili kwa vijana.

“Mimi nafikiri ule utaratibu wa kupiga viboko watoto pindi wanapokosea ungerejeshwa Kwani umekuwa ukisaidia sana malezi ya watoto lakini sasa hivi watoto wanakosea hata ukiwaelekeza hawaelewi na hatuwezi kuwachapa hii ni mbaya sana mimi nashauri viboko virudishwe,” amesema Mzee Dewji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles