21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 4, 2022

VIONGOZI VYAMA VYA UKOMBOZI WAMSIFU JPM

 

Na Mwandishi Wetu – Dar es Salaam      |        


VIONGOZI wa vyama vya siasa kutoka nchi 40 za Afrika, vikiwamo vyama vya ukombozi, wameipongeza Serikali ya Rais Dk. John Magufuli kwa juhudi za kuleta mageuzi ya kiuchumi na kuonyesha mfano wa mapambano dhidi ya rushwa.

Wametoa pongezi hizo katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Rais Magufuli baada ya mkutano maalumu wa majadiliano kati ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na vyama vya siasa takribani 40 vya Afrika, uliofanyika kwa siku mbili Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu jana, ilisema katika hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Chama cha SWAPO cha Namibia, Sophia Shaningwa, alimwelezea Rais Magufuli kama kiongozi shupavu aliyeonyesha mfano  katika mapambano dhidi ya rushwa, jitihada zake za kupigania rasilimali za taifa na kuwatetea wanyonge.

Naye kiongozi wa chama cha FLN cha Algeria, Said Lakhdari, aliipongeza China kwa uhusiano na ushirikiano wa karibu na Afrika na kuwasihi viongozi wa vyama vya siasa vya bara hilo kupigania amani.

Mapema akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM, Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho na Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda, alikishukuru Chama cha CPC kwa kudumisha uhusiano wake na Afrika na kuichagua Tanzania kuwa mahali pa kufanyia mkutano huo ambao umefanyika kwa mara ya kwanza nje ya China.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,654FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles