VIONGOZI KUAGA MWILI WA MKE WA DK. MWAKYEMBE

0
1106

 

LEONARD MANG’OHA Na CECILIA NGONYANI

-DAR ES SALAAM


MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassana, leo anatarajiwa kuwaongoza wananchi kuaga mwili wa   mke wa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Linah Mwakyembe aliyefariki dunia Julai 15, mwaka huu.

Mmoja wa wanakamati ya maandalizi ya mazishi ambaye hakufahamika jina lake mara moja, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa shughuli za kuaga mwili wa marehemu Linah zitaanza saa 3:00 asubuhi nyumbani kwa waziri huyo Kunduchi,  Dar es salaam.

Alisema baada ya mwili kuagwa,  saa 4:00 asubuhi utapelekwa katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika  Kunduchi kwa ibada na baadaye saa 7:00 mchana utapelekwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa safari ya kwenda Kyela mkoani Mbeya kwa mazishi yatakayofanyika kesho.

Wakati huohuo, viongozi mbalimbali wa serikali na siasa waliendelea kujitokeza nyumbani kwa waziri Mwakyembe kuomboeleza msiba huo.

Hao ni pamoja na na Rais Mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Ashantu Kijaji na Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva.

Wengine ni  Spika wa Bunge Mstaafu, Anne Makinda, Mbunge wa zamani wa Kahama, James Lembeli   na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya ITV na Radio One, Joyce Mhavile.

Mke wa Mwakyembe alifariki dunia Julai 15 katika hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam kwa   saratani ya matiti aliougua kwa miaka miwili na kutibiwa katika hospitali mbalimbali ndani na nje ya nchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here