25.5 C
Dar es Salaam
Thursday, September 28, 2023

Contact us: [email protected]

Viongozi Kilimanjaro watakiwa kufuatilia miradi ya maendeleo

Na Safina Sarwatt, Same

Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, imewataka Madiwani, Watendaji wa Kata na Vijiji kuhakikisha wanafuatilia kwa ukaribu miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali kwenye kila halmashauri ili kuzuia ubaadhilifu wa pesa.

Kauli hiyo imetolewa Jana Jnauari 2, na Kamati ya Siasa ya CCM, Mkoa wa Kilimanjaro wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo ili kujionea kwa macho utekelezaji wa ilani ya CCM, ikiwa ni maadhimisho ya mika 44 ya kuzaliwa kwa chama hicho.

Akitoa maelekezo hayo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi, amesema Madiwani, Watendaji Kata na Vijiji wanapaswa kuhakikisha kuwa wanakwenda kusimamia fedha za miradi ya serikali zinazotolewa ili miradi inayotekelezwa ndani ya kata husika inalinga na fedha halisi.

“Huko nyuma iko baadhi ya miradi ilikwama kutokana na viongozi hawa kutokufuatilia kwa ukaribu hivyo kuwataka kushirikiana na wataalamu ili kuhakikisha miradi hiyo inakuwa na ubora uliokusudiwa,”alisema Boisafi.

Kamati hiyo ilipata fursa ya kutembelea ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya Msingi Dindimo, shule ya msingi Bombo na shule ya sekondari Bombo, ujenzi wa mabweni, matundu 12 ambapo miradi hiyo ipo katika hatua za umaliziaji.

Vilevile kamati hiyo ilitembelea utekelezaji wa miradi ya (P4R), inayotekelezwa katika shule ya sekondari ya Bombo, kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo hususan katika nyanja ya elimu.

Kamati hiyo ilieleza kuwa imeridhishwa na hatua ya miradi hiyo na hivyo kutumia nafasi hiyo kumpongeza Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Same, Anastazia Tutuli, pamoja na Watendaji wake kwa kusimamia vema fedha za serikali zinazoletwa katika halmashauri hiyo kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo.

“Mkurugenzi na timu yako kwa hili tunakupongeza kwa kazi nzuri za usimamizi wa miradi ya maendeleo ndani ya halmashauri yako, miradi yote hii tumeitembelea na kujionea imejengwa katika ubora wa hali ya juu,”alisema Boisafi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Same, Anastazia Tutuli, amesema halmashauri hiyo inakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa 28 kwa upande wa shule za sekondari.

“Tuna uhaba wa vyumba 28 vya madarasa kwa upande wa shule za sekondari kati ya hivyo vyumba nane vimefikia kwenye lenta kwa ajili ya ukamilishaji,”alisema.

Ziara hiyo iIlihudhuriwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Jonathan Mabihya, viongozi wa kamati ya siasa mkoa, wakuu wa idara na vitengo na watendaji wa kata ambapo jumla ya miradi mitatu ya maendeleo ilikaguliwa ambayo ni ujenzi wa vyumba vya madarasa, hostel, mabweni na matundu ya vyoo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,750FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles