30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Viongozi Chadema watishia kuhama

Dk. Wilbrod Slaa
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa

Na Pendo Fundisha, Mbeya

BAADHI ya wanachama kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mbeya, wamesema wapo tayari kukihama chama hicho endapo uongozi wa juu utaendelea kuwakumbatia viongozi wa mikoa ambao wanaendesha shughuli za kichama kwa matakwa yao.

Wamesema viongozi hao wakishirikiana na baadhi ya viongozi ngazi Taifa, wamekuwa ni kero kwa wanachama wenzao kutokana na kufanya shughuli za kichama kama wanavyoziongoza familia zao nyumbani.

Wakizungumza na MTANZANIA jana kwa sharti la kutokutajwa majina, walisema chama kimekuwa kikiongozwa na katiba, lakini wanashangaa kuona baadhi ya shughuli zikiendeshwa kwa matakwa ya watu binafsi badala ya kufuata taratibu na miongozo iliyomo kwenye Katiba yao.

Akizungumzia mkakati wa chama hicho, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, alisema chama kinajipanga ili kuhakikisha mwakani kinaongoza halmashauri hiyo.

“Lengo letu kwa sasa ndani ya chama ni kukamata halmashauri, hivyo mikakati yetu ni kuchukua viti vingi ambavyo ndivyo vitasaidia kuongoza na kuondoa mianya yote ya rushwa,” alisema Mbilinyi.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Suala la majadiliano na maelewano nchini libebe taswira ya utaifa Rais, viongozi wa dini na watu wengi wenye mapeni mema wangefurahi endapo viongozi wote wa UKAWA mtakaa na kuweka mikakati bora ya kuenenda na Uandaaji wa Katiba bora ya Watanzania wote. Hakuna kitakachoshindikana mkikaa pamoja. leo Tanzania tutaingia kweli historia chafu endapo hapatakuwa na muafaka wakati mliochaguliwa mnadhamana ya kuwaandalia watanzania katiba bora. LEO vyama vipo hivi kesho watu wakaaanzisha vingine mliopo mkawa mkaungana kwenye dimbwi la upinzani. fikirini endapo Katiba haitakuwa nzuri mtaishi vipi kwenye mazingira ya Ushindani wa Kisiasa. Viongozi fikirini mbali kuwa leo huyu kesho yule wote mkiwa kwenye mazingira mazuri. Watoa matusi, kejeli na wabinafsi ni sumu katika mchakato toeni hoja wakati ni huu wa kujenga au kuharibu

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles