29.8 C
Dar es Salaam
Sunday, September 15, 2024

Contact us: [email protected]

VIONGOZI CHADEMA WARIPOTI POLISI, MBOWE MGONJWA

Na Leonard Mang’oha, Dar es Salaam

Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wameripoti Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam asubuhi hii huku Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, akishindwa kuripoti kutokana na ugonjwa.

Wakili wa Chadema), Alex Massaba, amesema Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, hawezi kuripoti Polisi kwa sababu anaumwa, hata hivyo hakuweka wazi ugonjwa anaoumwa

Viongozi hao wamewasili kituoni hapo kutokana na wito waliopewa wa kuripoti kituoni hapo wiki iliyopita na kutakiwa kurudi leo ambapo waliongozwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Vicent Mashinji.

Wengine walioripoti kituoni hapo hadi sasa ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na Mbunge wa wa Tarime Mjini, Esther Matiko, hadi sasa

Viongozi hao wamewasili kituoni hapo saa 1:25 asubuhi wakisindikizwa na Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles