31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

VIONGOZI CHADEMA WAPATA DHAMANA WAKIWA SELO, KURIPOTI POLISI KILA ALHAMISI

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Mahakama ya Hakimu ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewapatia dhamana viongozi sita wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), bila washtakiwa hao kuwapo mahakamani huku wakitakiwa kuripoti kila Alhamisi.

Awali, viongozi hao akiwamo Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, walidhaniwa kuletwa mahakamani hapo na mahakama ikaamua kuketi na mawakili wa pande zote mbili kujadili kama washtakiwa hao wataletwa au la ili itoe uamuzi wake.

Baada ya makubalianao hayo, Inspekta Shabani wa Magereza ameieleza mahakama kuwa washtakiwa hao wameshindwa kuletwa mahakamani hapo kwa sababu gari la kuwaleta ni bovu.

Akitoa uamuzi wake, Hakimu Mkazi Wilbard Mashauri amewataka washtakiwa hao kuwa wadhamini wawili kila mmoja na kusaini kwa maandishi ya Sh milioni 20.

“Kila mshtakiwa atasaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni 20, wadhamini pia watasaini kiwango hicho, washtakiwa wakiwa nje kwa dhamana wanatakiwa kuripoti polisi mara moja kwa wiki, ambayo ni kila siku ya Alhamisi,” amesema.

Pamoja na Mbowe, viongozi wengine ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Vincent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko ambao wanakabiliwa na mashtaka manane yakiwamo kuhamasisha maandamano, uchochezi na uasi.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles