25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 21, 2023

Contact us: [email protected]

Viongozi CCM wampokea kada Chadema

BENJAMIN MASESE -RORYA

ALIYEKUWA kada maarufu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Rorya, Godfrey Mirondo, amewatoa machozi ya furaha wanachama na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya kutangaza kujiunga na chama hicho.

Mirondo alijiunga CCM juzi na kupokewa na Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Rorya, Charles Ochele, wakati wa mkutano wa hadhara, Kijiji cha Nyamtinga.

Baadhi ya viongozi wakiongozwa na Diwani wa Kata ya Nyamtinga, Chacha Nyambaki, walishangilia kwa kunyosha mikono juu kama ishara ya kumshukuru Mungu na kwenda kumkumbatia Mirondo.

Akizungumza baada ya kupokewa, Mirondo alisema alichokuwa akikitafuta upande wa upinzani ni mabadiliko ya kweli yanayoleta maendeleo halisia kwa watu, hivyo amekoshwa na Rais Dk. John Magufuli alivyoibadilisha CCM na Serikali yake kuwatumikia wananchi.

“Nawashukuru viongozi wa CCM Wilaya ya Rorya kunipokea na sijashawishiwa na mtu kuja kwenu, isipokuwa mtazamo wangu na busara zangu, mimi ni msomi na najua nilichokuwa nakifanya na malengo yangu.

“Lakini imefika wakati nimeona njia iliyokuwa imezibwa na kusababisha nisifikie kile nilichokuwa nimekikusudia, imefunguliwa na Rais Magufuli.

 “Hivyo nawaomba wanachama wa Chadema ambao walikuwa wananikubali kisiasa na hata mtazamo na mawazo yangu, basi nawaomba mnifuate huku niliko au tushirikiane kwa moyo safi na bila ubaguzi mkiwa huko huko ikiwa lengo likiwa moja tu ni maendeleo kwa wote.

“Lakini kama ulikuwa unanifuata kwa itikadi za Chadema, naomba tuachane kuanzia leo,” alisema.

Kwa upande wake, Ochele alishukuru uamuzi wa kijana huyo msomi kutumia elimu yake kujitathmini upande aliokuwa akiupambania.

Diwani wa Kata ya Nyamtinga, Nyambaki, alisema amejisikia furaha ya kupitiliza kutokana na anavyokumbuka namna alivyopambana na Mirondo mwaka 2015, wakati wa kampeni za kugombea nafasi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles