24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Viongozi CCM Serengeti waguswa na ‘Futuru ya Samia’

Na Malima Lubasha, Serengeti

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Serengeti, Mrobanda Japan na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Ayubu Makuruma wameguswa na mpango wa futuru na Samia uliokutanisha watu mbalimbali kutoka madhehebu tofauti kufuturu pamoja.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Said Mohamed Mtanda ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara,aliandaa futari na kufuturisha waumini wa dini ya kiislamu na watu wengine serengeti mpango ulioitwa Futuru na Samia uliofadhiliwa na Benki ya Azania.

Akitoa salamu za chama wakati wa futari hiyo Mwenyeti wa CCM Wilaya Serengeti, Japan alisema mbele ya hadhara hiyo kuwa kitendo hicho ni cha kipekee kwake kukiona kwani kimewaleta watu pamoja bila kujali dini wala itikadi zao za vyama na kwamba hiyo kwake ni mara ya pili kushiriki.

“Natoa pongezi RC Mtanda ukiwa mkoani mara umefanya kazi ya kusimamia ilani ya CCM, sikupenda uhame lakini kwa kuwa taratibu za serikali, sina pingamizi  nakutakia mafanikio mema huko Mwanza na hili jambo kutukutanisha hapa kupata futari ni jambo la pekee Mungu akubariki sana,”amesema Japan.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti,Ayubu Makuruma,amesema kwake hiyo ni mara ya kwanza kushiriki futari na waumini na kwamba ameguswa sana na kitendo hicho.

“ Dini zote wilayani hapa ziendelee kushirikiana katika shughuli mbalimbali za maendeleo kwani jambo hili la kutukutanisha pamoja kufuturu ni jambo la kheri pia pongezi za pekee kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza awali alikuwa Mara kwa kazi nzuri uliyofanya kuwaletea maendeleo wananchi na jambo zuri ni hili lililotukutanisha hapa,”amesema Makuruma. 

Aidha, Sheikhe wa Wilaya hiyo, Juma Simba amewataka wale wote wenye nia ya kufuturisha waislamu mwezi wa Ramadhan wafike ofisi za BAKWATA kupata taratibu.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara Azania Benki, Dk. Rhimo Nyansaho,akitoa salaamu za benki hiyo amesema kuandaa futari hiyo walishirikishwa na Mkuu wa Mkoa na walikubali kama taasisi ya fedha ili jamii iweze kukutana na kushiriki pamoja kufuturu bila kujali imani za dini na wameonyesha umoja,amani na mshikamano.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles