24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Viongozi Amcos wadaiwa kutumia fedha za wakulima pamba kutengeneza barabara

DERICK MILTON-MEATU

MKUU wa Wilaya ya Meatu, Mkoani Simiyu Dk. Joseph Chilongani ameagiza kukamatwa mara moja kwa viongozi wa chama cha msingi cha ushirika (Amcos) Sapa, wanaotuhumiwa kutumia fedha za malipo ya wakulima wa pamba kutengeneza barabara.

Amcos hiyo ambayo ipo kwenye kijiji cha Sapa wilayani humo, na viongozi wake wanadaiwa kutumia kiasi cha sh. milioni 1.8 fedha ambazo zilipelekwa na wanunuzi wa pamba kwa ajili ya kulipa madeni ya wakulima.

Dk. Chilongani alitoa agizo hilo jana mbele za viongozi wa vyama vya ushirika wilayani humo wakati wa kikao chake na viongozi hao ambacho kilikuwa maalumu kujadili changamoto zilizojitokeza katika msimu uliopita wa zao hilo.

Mbali na agizo hilo mkuu huyo wa wilaya aligiza pia, kukamatwa kwa viongozi wa Amcos ya Ilamba ndogo, wanaotuhumiwa kutumia kiasi cha Sh. milioni 27.5 za wakulima kwa matumizi yao binafsi.

Kiongozi huyo alitoa maagizo hayo kwa Mkuu wa polisi wa wilaya hiyo (OCD) pamoja na Ofisa Ushirika wa halmashauri, Godfrey Sekajingo, ambapo alitoa muda wa siku tatu kwa watuhumiwa hao wawe wamerejesha fedha hizo.

Hatua ya Mkuu huyo wa Wilaya ilikuja baada ya ofisa ushirika huyo kutoa taarifa ya msimu huo uliopita wa pamba, ambapo alisema kati ya Amcos 84 zilizoko wilayani humo, mbili ndizo zilikutwa na matatizo ya matumizi mabaya ya fedha.

Lekajingo alisema kuwa viongozi wa Amcos wa Sapa, waliamua kutumia fedha hizo za wakulima kutengeneza barabara yenye urefu wa zaidi ya mita 100 ili magari yanayosomba pamba  yaweze kupita vizuri.

“ Wakati tunawahoji hao viongozi walisema barabara hiyo ilisababisha wanunuzi wengi kugoma kwenda kuchukua pamba, ndipo wakaamua kutumia fedha hizo za wakulima kutengeneza ili magari yaweze kupita na kuchukua pamba,” Alisema Lakajingo.

Alisema kitendo kilichofanywa na viongozi hao ni kinyume cha utaratibu, kwani mwenye mamlaka ya kutengeneza bBarabara ni Wakala wa barabara vijijini (Tarula) hivyo walitakiwa kutoa taarifa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ili aweze kuwaagiza Tarula wakafanye matengenezo.

Kuhusu Amcos ya Ilamba ndogo, Ofisa Ushirika huyo alisema kuwa viongozi hao walitumia milioni 27.5 fedha za malipo ya wakulima kufanya kazi zao binafsi, huku akibainisha kuwa wakulima wa wilaya hiyo wanadai zaidi ya sh. bilioni nne.

Mkuu huyo wa Wilaya mbali na kuagiza kukamatwa viongozi hao, aliwataka pia kuzirejesha fedha hizo mara moja, huku akiwataka viongozi wengine wa Amcos kuwa makini na fedha za wakulima.

Wakati huo huo Bodi ya Pamba nchini imewatoa hofu wakulima wa zao hilo katika Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu, juu ya upatikanaji wa mbegu kuelekea msimu mpya wa kilimo ambao tayari umeanza.

Akizungumza na wakulima wa zao hilo katika vijiji vya Isengwa na Mwandoya Wilayani huo, pamoja na kamati ya mazao ya wilaya, Mkaguzi wa pamba kutoka bodi hiyo wilaya, Jeremiah Kalissa alisema mbegu zipo za kutosha.

Alisema bodi hiyo itahakikisha kila mkulima mwenye kuhitaji kulima pamba anapatiwa mbegu za kutosha eneo lake la kilimo, hata kama hatakuwa na uwezo wa kununua.

Kalissa alisema jumla ya kampuni sita za pamba zimepewa kazi ya kusambaza mbegu kwa wakulima, ambapo kati ya tani 2,290 zinazohitajika kwenye wilaya hiyo tani 1850 tayari zimesambazwa kwa wakulima.

Alisema kuwa ndani ya wiki moja mbegu nyingine ambazo bado hazijasambazwa zitakuwa tayari zimewafikia wakulima, kwani baadhi ya kampuni zinaendelea na zoezi la upakiaji.

Alisema awali mahitaji ya mbegu kwenye wilaya hiyo yalikuwa tani 2100, na baada ya kuanza kusambaza yameongezeka hadi kufikia tani 2,290 ongezeko la tani 190.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles