29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Viongozi Afrika kushiriki mazishi ya Tshisekedi

KINSHASA, DRC

MWILI wa aliyekuwa kiongozi mkuu wa upinzani na waziri mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Etienne Tshisekedi, umewasili jijini Kinshasa na jana wananchi walitoa heshima zao za mwisho.

Mwili wa Tshisekedi uliwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kinshasa na kupokelewa na viongozi kadhaa wa Serikali pamoja na wananchi waliokuwa nje ya uwanja kusubiri mwili wake.

Tshisekedi alifariki akiwa mjini Brussels Februari mwaka 2017 akiwa na umri wa miaka 84, ambapo ameshindwa kushuhudia kuapishwa kwa mwanawe, Felix Tshisekedi, ambaye amekuwa Rais wa DRC kupitia uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Felix aliahidi kuurejesha nyumbani mwili wa baba yake na kuuzika katika eneo linalostahili, akitimiza ahadi ambayo alishindwa kuifanya wakati wa utawala wa Rais Joseph Kabila.

Baada ya kuchelewa kuondoka mjini Brussels, hatimaye juzi mwili wake ulisafirisha na kuwasili jijini Kinshasa. Mtoto wake, Felix aliongoza ujumbe wa viongozi wengine kuupokea mwili wa baba yake.

Jeneza jeupe lililofunikwa na bendera za taifa, lilitolewa katika ndege na askari kuupokea na kisha kuupakia kwenye gari maalumu.

Mwili wa Tshisekedi umewekwa katika uwanja wa mpira wa Stade Martyr, ambako wananchi walipata nafasi ya kutoa heshima za mwisho kabla ya mazishi yake hapo kesho kwenye mji wa Nsele, nje kidogo ya jiji la Kinshasa.

Jumla ya viongozi 6 wa Afrika wanatarajiwa kuhudhuria mazishi yake, akiwamo Rais wa Angola, Rais wa Rwanda, Paul Kagame, Rais wa Togo na nchi jirani ya Congo Brazzaville.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles