30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

VIONGOZI 160 KANDA YA ZIWA BADO HAWAJATANGAZA MALI ZAO

Na CLARA MATIMO-MWANZA

JUMLA ya viongozi 160 wa kada za utumishi wa umma pamoja na kada ya siasa kutoka Kanda ya Ziwa, bado hawajatekeleza takwa la kisheria linalowataka kutoa tamko la mali na madeni yao kwa kipindi kinachoishia Desemba 31, mwaka 2016.

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Msaidizi wa Sekretarieti ya Maadili ya  Viongozi wa Umma Kanda ya Ziwa, Fabian Pokela, iliyotolewa jana kwa gazeti hili, kati ya viongozi wa utumishi wa umma ambao hawajawasilisha tamko ni 122 kati ya 195 huku ikieleza viongozi wanasiasa 38 kati ya 926 nao walikuwa bado hivyo jumla yao kuwa 160.

Taarifa hiyo ya Pokela ilisema kiongozi yeyote anapaswa kutoa tamko lake la mali na madeni aliyonayo ndani ya siku 30 kuanzia siku anapochaguliwa au kuteuliwa katika wadhifa wake wa uongozi na baada ya kutekeleza takwa hilo la kisheria kila baada ya mwaka mmoja anapaswa kutoa tamko upya.

“Kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi  wa Umma namba 13 ya mwaka 1995 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2016, kutotoa au kuchelewa kutoa tamko  ni kosa la ukiukwaji wa maadili ya uongozi,” ilieleza taarifa hiyo.

 Taarifa hiyo ilifafanua kuwa sehemu ya (8) ya sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, kiongozi ambaye hatawasilisha tamko lake kwa wakati akithibitika kuwa na hatia, anastahili adhabu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuondolewa katika nafasi yake ya uongozi, kushushwa cheo, kufukuzwa kazi, kuonywa na pia kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria na kanuni nyingine husika.

“Endapo kiongozi wa siasa atabainika kuwa ametenda kosa la kiuadilifu kwa mujibu wa katiba, hatapaswa kugombea nafasi yoyote ya kisiasa kwa kipindi cha miaka mitano tokea alipokutwa na kosa hilo la kukiuka sheria ya maadili ya viongozi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles