26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 27, 2021

VIKWAZO VISIVYO NA TIJA KUNAIPOTEZEA NCHI UWEZO WA KUJIENDELEZA

Katika maisha yangu nimekutana na watu mbalimbali, nimeishi na wengi, na kufanya kazi na watu wa aina tofauti wenye hisia na tabia tofauti. Nimesoma na wengi kama upinde wa mvua wenye kabila, dini, imani na jinsia mbalimbali wenye mitindo na mtazamo mbali mbali kimaisha.

Nimekutana na watu wenye ujuzi na taaluma mbalimbali, wenye uwezo tofauti na uwezo wa akili kupita kiasi cha binadamu wa kawaida. Hii katika maisha yangu imenipa uzoefu mkubwa na wa kina kuweza kupambana na hali yeyoto ile. Maisha yangu ni kama maji kwenye mto ambayo unazunguka kuelekea kwenye maziwa au bahari. Vitu fulani fulani huwa daima vinajitokeza katika maisha yangu na wengine wengi. 

Huwa vinaibuka na kuja juu na kutufungua macho kwa wale tunaokutana nao na kujenga ushirikiano. Kwa mtu binafsi kuweza kutafuta mazingira mazuri ya kujiendeleza au kusaidia jamii si rahisi kama utakutana na changamoto mbali mbali ambazo zinakurudisha nyuma kwa sababu za hisia za watu ambao badala ya kukusaidia wanaweka maslahi yao mbele. Wema na uwezo wa kujua, kuelewa na kushughulikia hisia ni sifa huwezi kujifunza au kufundishwa, wewe ni mzaliwa na hayo.

Aidha una au hauna. ukosefu wa sifa hizi si mbaya tu ndio msingi wa kwamba kukumbana na utunzaji wa mifumo mingine ya kihisia na kiakili itakuwa changamoto. Hii inaweza kubuniwa kwa kufichwa  kiakili kliniki na aproni bandia hisia zako, lakini ukweli unabakia, ukosefu wa uwezo  yanahusiana na kuunganisha maarifa unaopatikana kwa kutokea maisha halisi ya hisia za watu na ubinadamu, nguvu kutaabika za uhusiano wa aina tofauti. Si lazima manufaa na ni mapambano kati ya haja ya kudhibiti na kuwa kueleweka. Mimi bado hujifunza mengi, maisha ni dhana na nahitaji bado kujifunza na kuwa na uzoefu zaidi.

Miundo ndani ya dhana yetu tunayoishi imebadilika sana na hasa mazingira ya ndani ya biashara na maisha ya watu wa kawaida. Kwa kurejesha na kuleta utulivu na imani kwenye nchi nyingi basi moja ya mbinu ni kushughulisha sana wazawa katika fursa ambazo zinajitokeza sehemu zingine za duniani kuhalalisha matukio ya ndani. Ukuaji wa uchumi kupungua au kusimama basi watu binafsi na vikundi vidogo vidogo vinawezeshwa. Wakati huo huo teknolojia ya kidigitali inakua na kuendelea kwa kasi kubwa kweli, malumbano na migogoro juu ya maadili na watu kutokuelewa na kutokuwa karibu na Serikali yao au utawala ni jambo ambalo linaonyesha kwamba maendeleo ya kifikra bado ni changamoto.

Hisia zinaunganishwa sana na matukio ya kwenye masoko kuliko kuona mbali na kuelekea kwamba msingi unaowekwa leo ni mavuno ya baadaye. Utaona mbali kama unajipanga na una chombo ambacho kinakusanya bila ya kubagua, kinachambua, kinaunganisha na kinajumuisha mitazamo mingi na kina uwezo wa kukusanya mawazo ya wengi wenye uzoefu tofauti na kutengeneza msingi bora. Hapa si mawazo na fikra za mtu binafsi bali ni mawazo ya wote yanawekwa pamoja na kutengeneza hicho kiunganishi. 

Chombo hicho kinawezesha uhusiano na mawasiliano ya kibiashara. Nchi kama Tanzania yenye baadhi ya watu wake wanaishi nje na kufanya kazi au kusoma ni rasilimali kubwa sana ambayo ikitumiwa vizuri italeta matunda mengi sana. Huko tu waliko ni wako kwenye masoko makubwa ambapo uchumi na kipato cha mtu wa kawaida kinazidi mara nyingi sana kipato cha mtu wa kawaida Tanzania.

Hilo la nje ni soko na ni fursa. Je wadau mbalimbali watawezaje kutumia fulsa hiyo kuleta mafanikio kwa jamaa zao? Watawezaje kutumiwa? Ni wanadiaspora kujipanga na kushirikiana na wadau ambao wapo ndani ya nchi na kushirikiana kwa kubadilishana ujuzi, kuelimishana na kujanyua werevu wa wote kuhusu mazingira yaliyopo.

Ili kuweza kutumia nafasi hiyo kuzalisha kwa ajili ya masoko hayo. Haya yote yanawezekana kama mazingira na miundombinu inawekwa kwa kurahisisha mawasiliano kati ya hizi jamii zetu za ndani na za nje. Wanadiaspora wanaleta nini? Wanaleta ujuzi, uelewa wa fikra za wakazi na jamii za Ulaya na sehemu zingine duniani, ufadhili wa kimawazo na fedha. Hizi zote ni baadhi tu ya mambo ambayo tunaweza kufanya pamoja. 

Huu ni ushauri wa bure kutoka kwangu lakini si mie tu ambaye nina fikra kama hizi ni wengi katika jamii ya Diaspora. Lakini tunaelewa kabisa kujipanga kwetu ni msingi wa kufanikiwa. Hisia zetu ambazo zinaweza kutukwamisha kwa sababu mbalimbali tuziweke pembeni. 

Na hapa nazungumzia hisia anbazo hazileti tija. Kuweka vikwazo ambavyo havina msingi ni kuipotezea nchi ule uwezo wa kujiendeleza. Kila mtu anahitajika uwe unaishi nchini au nje. 

Ukishafahamu hilo basi nikujipanga tu na kufanya yale uliyoyapanga kuyatekeleza

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,371FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles