25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, December 8, 2022

Contact us: [email protected]

‘Vijana wenye miaka 18 wanaongoza kwa ajali’

1455026805898

NA CHRISTINA GAULUHANGA, DAR ES SALAAM

MWENYEKITI wa Kamati ya Maadhimisho ya Usalama Barabarani, Henry Bantu amesema ajali nyingi zinazotokea nchini zinasababishwa na vijana wenye umri kati ya miaka 18 hadi 35.

Alikuwa akizungumza jana katika mafunzo ya Usalama Barabarani yaliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa) na kufadhiliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), kupitia Umoja wa Mataifa (UN),

Bantu alisema ipo haja ya kudhibiti ajali hizo kwa kuweka sheria ambazo zitawabana madereva kwa kigezo cha umri hasa wanaoendesha mabasi ya abiria.

Alisema limekuwa jambo la kawaida kwa wamiliki wengi kuwakabidhi madereva magari ya abiria bila kuzingatia uzoefu, umri na uwezo walionao wa taaluma hiyo.

“Limekuwa jambo la kawaida madereva wengi kukaa pale stendi ya Ubungo kusubiri neema ya kuteuliwa na matajiri kupewa gari  aende mikoani jambo ambalo linazidi kuchangia ongezeko la ajali,” alisema Bantu.

Alisema ni vema wamiliki wa magari kuzingatia aina ya matairi ya magari wanayonunua yaweze kulingana na barabara kupunguza ajali zinazotokea kwa uzembe.

Bantu alisema  usalama barabarani uanze kwa madereva wenyewe kujihami kwa kuangalia hatari zilizopo mbele na zinazotegemewa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,682FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles