25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

Vijana wanyooshewa kidole kwa kutokuwa tayari kushiriki shughuli za maendeleo

Na AMINA OMARI-TANGA

Imeelezwa kuwa kutokuwa na utayari kwa vijana kumesababisha kutoshirikishwa  kwenye shughuli za maendeleo na kuishia kulalamika.

Hayo yamesemwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga, Mustafa Seleboss wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha kujadili uanzishwajiwa mabaraza ya Vijana ngazi ya kata. 

Alisema licha ya Serikali kuweka sera nzuri ya uwezeshaji kwa vijana lakini kutokana na wao kutaka matokeo ya haraka wameshindwa kuendana na utekelezaji wa sera hiyo.

“Pale Halmashauri tunatoa kila baada ya miezi mitatu mikopo kwa makundi maalum lakini kila siku fedha za mikopo ya vijana zinarudi kutokana na kutokuwa na utayari wa kuja na mawazo yatakayowawezesha kupata mikopo hiyo,” alisema Meya huyo.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Kiona Youth ambayo inasimamia mradi wa uanzishwaji wa mabaraza hayo, Fatma Fungo alisema kupitia mabaraza hayo vijana wataweza kupata sehemu ya kuwasilisha changamoto zao.

Alisema uanzishwaji wa mabaraza ngazi ya kata itakuwa ni sehemu nzuri ya kuunganisha mawazo na mitazamo ya vijana hadi kufikia ngazi ya Taifa na kuweza kupatiwa ufumbuzi wa haraka na mamlaka husika.

“Tumeona badala ya vijana kuendelea kulalamika tuu mitaani tumekuja na mradi huu ambao utaweza kusaidia kupata mahali pa kusema na fursa ya kupata viongozi watakaoweza kuwasemea vijana”alisema Fungo.

Ofisa Vijana wa Jiji la Tanga, Omari Ali alisema mabaraza hayo ni sehemu sahihi ya kutoa maoni yao na mawazo juu ya kinachofanywa na Serikali yao.

“Ni sehemu pekee ya kujua changamoto za vijana na mahali pa kupaza sauti na kuweza kufanyiwa kazi kwa urahisi na uongozi wa Serikali,” alisema Ali.

Jumla ya kata tano za Tangasisi, Central,Ngamiani Kati, Nguvumali na Maweni zipo kwenye majaribio ya kuanzishwa kwa mabaraza ya kata katika Jiji la Tanga.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,301FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles