31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Vijana, wanawake na walemavu wasisahaulike Uchaguzi Mkuu 2020

Na ASHA BANI
TAFITI mbalimbali na uhalisia uliopo ni kwamba kuna makundi maalumu ya watu wanasahaulika katika kipindi cha uchaguzi.
Uchaguzi huo uwe mdogo ama mkubwa, lakini makundi hayo yameonyesha kutopewa kipaumbele cha kipekee ili kuweza kushiriki kikamilifu.


Makundi hayo ni ya vijana, wanawake na walemavu ambayo yameelezwa kuwa ushirikishwaji wao katika masuala ya uchaguzi hauwafikii kwa wakati sahihi.


Pia tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa makundi hayo ushirikishwaji wao katika uchaguzi unawafikia mwishoni na sio mwanzoni pindi mchakato unapoanza.


Hivyo basi, kama wadau mbalimbali ni muda mwafaka sasa kabla ya kuelekea katika uchaguzi mkuu kuyapa ushirikiano makundi yote kwa usawa ili yashiriki kikamilifu katika uchaguzi.


Ushirikishwaji huo mdogo pia umezungumziwa na Mkurugenzi wa Shirika la Vijana linalowajengea uwezo katika ushiriki wa mambo mbalimbali ikiwemo kisera na kisiasa la TYC, Lenin Kazoba anasema  vyama vya siasa vinapaswa kuweka mkakati wa kuhakikisha makundi hayo yanashirikishwa ipasavyo na kupatiwa nafasi katika chaguzi mbalimbali ikiwemo Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika mwaka huu.


Ushauri uliotolewa na TYC wa kuvitaka vyama vya siasa kutilia mkazo makundi hayo ikiwa ni pamoja na kupewa kipaumbele katika ushirikishaji wa mchakato wa  uchaguzi unapoanzia ikiwemo mchakato wa uchukuaji wa fomu za uchaguzi, utekelezwe kwa wadau mbalimbali wa vyama vya siasa nchini.

TYC inasema imefanya utafiti huo katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka jana, ambao ulikuwa na lengo la kupata maoni mbalimbali juu ya makundi hayo na ulilenga  wilaya mbili za Ubungo na Kigamboni.


Kazoba anasema kutokana na wilaya hizo kuwa mpya waliangalia ni namna gani wataweza kujifunza vitu katika  uchaguzi  huo na kuvifanya visiweze kujirudia katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba.
Hivyo basi, ni vyema suala hilo kwa sasa likaondolewa na makundi maalumu yakajitokeza na kugombea huku yakipewa sapoti.

Changamoto mbalimbali zilizojitokeza kwa upande wao ikiwemo utoaji wa elimu katika makundi hayo zisije kujirudia tena kwani zitakuwa zinabagua makundi hayo maalumu.


Kazoba anasema katika uchaguzi wa mwaka huu wamejipanga vema kuhamasisha ushiriki wa makundi haya katika kuingia kwenye vinyang’anyiro vya viti vya ubunge  na udiwani.


Na si tu asasi za kiraia, lakini ni vyema kwa wadau mbalimbali waweze kushiriki katika kuhakikisha makundi hayo yanavutiwa na sera zao, kupewa nafasi za upendeleo na hata kusimamia sheria zilizopo kwa uwazi ili kuweza kupata nafasi za kugombea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles