29.8 C
Dar es Salaam
Sunday, September 15, 2024

Contact us: [email protected]

Vijana waliopata mafunzo JKT waandamana

Pg 1Na Asifiwe George, Dar es Salaam,
VIJANA zaidi ya 300 waliopata mafunzo kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wameandamana kwenda Ikulu kumwona Rais Jakaya Kikwete ili asikilize kilio chao na kupinga upendeleo wa ajira ndani ya jeshi.
Maandamano hayo yalifanyika jijini Dar es Salaam jana kwa saa mbili asubuhi kwa vijana hao kujikusanya katika eneo la Jangwani huku wakiwa wameshika bendera nyekundu kupita barabara ya Morogoro, Umoja wa Mataifa hadi Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR).
Vijana hao baada ya kufikia katika eneo hilo walizuiwa na askari polisi waliokuwa wameweka ulinzi maalumu huku wakiwataka kueleza matatizo yao kwani si kila jambo linapaswa kufanywa maandamano, mengine yanaweza kuzungumzwa.
Mmoja wa vijana hao aliyejitambulisha kwa jina la Magesa Masatu, alisema lengo la maandamano hayo ni kupeleka kilio chao kwa Rais Kikwete baada ya kukosa ajira kwa muda mrefu ndani ya jeshi.
Alisema walifikia uamuzi huo baada ya kupeleka barua za maombi ya kazi Wizara ya Kazi na Ajira, Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Ulinzi bila kupatiwa ufumbuzi wowote.
“Vijana wengi wamekuwa wakipelekwa JKT na kuahidiwa kupatiwa ajira, lakini toka mwaka 2000 hadi 2014 wameajiriwa vijana wachache na wengine tumekuwa tukiachwa.
“Kama Serikali haina uwezo wa kuajiri vijana kwanini wanatupeleka JKT na kutupatia mafunzo ambayo wanajua kuwa baadaye tunaweza tukayatumia vibaya kutokana tatizo la ukosefu wa ajira?
“Wengi hatuna kazi tunaishia kuzurura mitaani bila kazi yoyote, kutokana na hali hii mafunzo tuliyopewa yanaweza yakasababisha vijana wengi kufanya mambo ambayo baadaye yataleta adhari kwa taifa,” alisema Masatu.
Kwa upande wake Fabian Mashauri alisema wasipopata majibu mazuri kutoka kwa Rais Kikwete wataendelea kupigania haki yao hadi pale itakapopatikana. Pia alisema Serikali isipoangalia suala hilo la vijana, watakuwa wanatengeneza makundi hatarishi ambayo yatakuja kuliathiri taifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles