26.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Vijana waaswa kufanya kazi kwa bidii

Brighiter Masaki

MKURUGENZI wa idara ya elimu na mawasiliano, jimbo la Kusini, Abraham Youze, amewataka vijana kufanya kazi kwa bidii ili kujikwamua kiuchumi na kuwa chachu ya maendeleo katika Taifa.

Hayo ameyasema katika usharika wa Mbagala, jijini Dar es Salaam, akifungua kongomano la makambi ya dhehebu la Adventista Wasabato, amesema kijana yeyote anatakiwa kufanyakazi kwa bidii ili aweze kumtumikia Mungu kikamilifu.

“Kijana lazima awe na kazi ya kufanya, ndiyo sababu kubwa hata hapa kanisani huwa tunatoa elimu ya ujasiriamali, hata vitabu vya dini vimeandika asiyefanya kazi na asile, na kwa wenzetu waislamu pia wanazo nguzo tano, lazima kusali, kutoa sadaka pamoja na kwenda kuhiji huwezi kwenda kuhiji kama hauna pesa,” anasema Youze.

Aidha aliongeza kuwa vijana wanatakiwa kuwa wahaminifu, uhadilifu katika kulinda na kutunza ushuhuda wao machoni pa watu na kuwa waaminifu mbele za Mungu na kumshukuru Rais kwa kufanya nchi yetu kuwa na uhuru wa dini, ndo mana unakuta saizi tuko hapa tunapata nafasi ya kuwa pamoja

Mchungaji, Christian Kivuyo, naye alisema kongamano hilo litafanyika kwa wiki nzima, kwa mwaka, huwakutanisha waumini wa dhehebu hilo na madhehebu mengine kusheherekea na kujifunza neno la Mungu na fursa mbalimbali bila kujali dini au kabila gani mtu anatoka.

“Mikutano hii huwa inachukuwa watu wa namna yoyote kwa sababu ndani yake siyo tu kwamba huwa kuna neno la Mungu bali kunakuwa na mafundisho mbalimbali kama semina za ndoa, uhusiano wa vijana na uchumba, jinsi gani anaweza kuishi katika uchumba” alisema Mchungaji Kivuyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,206FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles