23 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Vijana Siha wapatiwa bodaboda kujikwamua kiuchumi

Safina Sarwatt, Siha



Zaidi vikundi 10 vya vijana katika Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, vimekabidhiwa pikipiki na fedha taslimu Sh milioni 2.4 na kiongozi wa mbio za Mwenge Taifa, Francis Kabeho, kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.

Fedha hizo ni zile zinazotokana na mapato ya ndani ya halmashauri kwa ajili ya mikopo ya akina mama, vijana na walemavu.

Akikabidhi kwa vijana hao, Kabeho aliipongeza halmashauri hiyo kutenga fedha kwa ajili ya kuwawezesha vikundi ya vijana.

“Ni vema sasa vijana wakatumia fursa hizo katika kujikwamua kiuchumi na kuondokana na hali ya umaskini na tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana nchini,” amesema.

Kabeho amesema Tanzania kwa sasa ina wasomi wengi huku ajira zikiwa chache ambapo amewataka vijana kutambua fursa mbalimbali za kuzalisha ajira badala  ya kutegemea ajira katika taasisi za serikali na binafsi.

Awali akizungumza Mkurugenzi wa Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha, Valerian Juwal, alisema katika mikopo iliyotolewa, vikundi vitano kati ya vikundi 10 vilipatiwa mkopo wa pikipiki  za biashara (bodaboda) na vikundi vingine vitano vimepatiwa mikopo fedha.

Mwenge wa uhuru ukiwa Wilaya ya Siha umezindua  miradi mitano ya maendeleo yenye thamani ya Sh milioni  491.5.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles