23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

VIJANA NCHINI WAZIDI KUWA TEGEMEZI

Na JOHANES RESPICHIUS-DAR ES SALAAM

ASILIMIA 64 ya vijana 2,000 waliofanyiwa utafiti nchi nzima hawana uhakika wa kupata fedha za kujikimu  na hawajui watakula nini kila wakiamka.

Mratibu wa Utafiti wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Well Told Story kupitia mradi wa Shujaaz, Winnie Nyato, alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa lengo la tafiti hizo ni kuleta matokeo chanya kwa vijana.

Alisema kwamba haiwezekani kufanya jitihada za kuwafikia vijana bila kujua matatizo yao ndiyo maana wamefanya  tafiti hizo ili kama wakitaka kuwasaidia kwa namna moja au nyingine wawe wanajua undani wao.

“Tumebaini kuwa wastani wa asilimia 64 ya vijana wa umri wa miaka 15 hadi 24 huamka asubuhi bila wao kujua watakula nini au watatumia usafiri gani kwenda sehemu fulani.

“Kwa hiyo vijana wengi hawajajidhatiti kifedha kuweza kumudu mahitaji yao ya siku na mwaka huu hali imezidi kuwa mbaya zaidi kulinganisha mwaka jana ambapo ilikuwa asilimia 52,” alisema Nyato.

Nyato alisema vijana  wenye uhakika wa kumudu  mahitaji yao ya siku nzima idadi imepungua kutoka asilimia saba hadi tatu.

Alisema utafiti hu umehusisha mikoa yote ya Tanzania bara.

Wakati huo huo, Mkuu wa Kitengo cha Utafiti cha taaisi hiyo, Dk Anastasia Mirzoyants, alisema utafiti waliofanya katika sekta ya kilimo wamebaini asilimia 51 ya vijana waishio mjini na vijijini wanajihusisha na kilimo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles