29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

VIGOGO WAMUAGA MKE WA DK MWAKYEMBE

KWAHERI: Rais mstaafu Benjamin Mkapa, akitoa heshima za mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa Linah Mwakyembe, aliyekuwa mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, wakati wa ibada ya kumuaga iliyofanyika Kanisa la KKKT Usharika wa Kunduchi, Dar es Salaam jana kabla ya kusafirishwa kwenda Kyela mkoani Mbeya kwa mazishi. PICHA: SILVAN KIWALE

LEONARD MANG’OHA na MWANAIDI MZIRAY (TSJ)

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Marais Wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa, jana waliongoza mamia ya wananchi kuaga mwili wa Linah, mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe.

Viongozi wengine waliojitokeza katika misa takatifu iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Kunduchi Dar es Salaam ni   Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, Jaji Kiongozi, Fredinand Wambali na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju.

Katika orodha hiyo wamo pia Spika wa Bunge Mstaafu, Anne Makinda, Mwenyekiti wa Bunge, Azzan Zungu, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole na Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Paramagamba Kabudi, wabunge na viongozi mbalimbali wa serikali.

Akizungumza wakati wa misa hiyo, Samia alisema pamoja na jitihada za binadamu kujitahidi kuokoa maisha ya wapendwa wao lakini hazizuii kudra za Mwenyezi Mungu.

Alisema Dk. Mwakyembe alijitahidi kuokoa maisha ya mkewe Linah, lakini Mungu ndiye mpangaji wa kila kitu.

“Tunatambua Linah alikuwa mshauri na mpangaji wako lakini tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kutupatia zawadi ya Linah na tumshukuru pia kwa kumchukuwa mja wake.

“Mahubiri yaliyotolewa hapa yametufunza Mungu anakupa mwenza unajenga mazoea naye, lakini hujui lini anamchukua,” alisema Samia.

Msemaji wa Serikali katika misa hiyo, Profesa Kabudi, alisema serikali iko pamoja na Waziri Mwakyembe  na familia yake katika kapindi hiki kigumu na chenye majonzi.

“Pamoja na kuuguliwa na mkeo kwa muda mrefu lakini uliendelea kutekeleza majukumu yako ya serikali na hata aliyekuona hivi karibuni asingeweza kubaini kama unauguza,” alisema Profesa Kabudi.

Akitoa mahubiri katika idaba hiyo, Mchungaji Chediel Lwiza alisema marehemu alijitoa kwa nafasi na kipawa chake vizuri kwa sababu alimpenda Mungu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles